Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mbinu za kiasili ni muarobaini wa kukabili mabadiliko ya tabianchi- UNEP

Mbinu za kiasili ni muarobaini wa kukabili mabadiliko ya tabianchi- UNEP

Pakua

Karibu robo tatu ya mataifa kote duniani yameweka mipango ya kukabiliana na kuhimili mabadiliko ya tabianchi, lakini ufadhili na utekelezaji unaohitajika wa mipango hiyo ndio mtihani mkubwa kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP. Grace Kaneiya na maelezo zaidi.

Ripoti hiyo “Mapengo ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi ya mwaka 2020” inasema kila mwaka gharama za kuhimi mabadiliko ya tabianchi katika mataifa yanayoendelea inakadiriwa kuwa dola bilioni 70 huku kiwango hicho kikitarajiwa kuongezeka na kufikia kati yad ola bilioni 140-300 ifikapo mwaka 2050 na kati ya dola bilioni 280-500 mwaka 2050. 

Hivyo ripoti imeonya na kusisitiza kwamba “Suluhu za kiasili ni muhimu katika kujenga mnepo na kuhimili kishindo hicho na zinahitaji kupewa kipaumbele cha juu hasa wakati huu ambapo ongezeko la joto linaendelea na athari za mabadiliko ya tabianchi zinaongezeka. Nchi ni lazima kuongeze hatua zake haraka kuhimili hali mpya ya maisha, la sivyo zikabiliwe na hasara kubwa, uharibifu na kupoteza maisha ya watu.” 

Matakwa ya mkataba wa Paris 

Kwa nchi na jamii kujenga mnepo ili ziweze kuhimili athari za mabadiliko hayo ni nguzo muhimu katika mkutano wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi.  

Mkataba huo unazitaka nchi zote zilizotyia saini kutekeleza hatua za kujenga mnepo na kuhimu mabadailiko ta tabianchi kupitia mikakati ya kitaifa, mifumo ya taarifa ya mabadiliko ya tabianchi, utoaji wa tahadhari mapema, hatua za kujilinda na uwekezaji katika mustakbali unaojali mazingira. 

Pia ripoti imetaka ufadhili wa umma na binafsi kwa ajili ya mikakati ya kuhimili uongezwe haraka pamoja na utekelezaji wake. 

Nazo suluhu za asili za kushughulikia mabadiliko ya kijamii, kuleta ustawi wa binadamu na faida za bayoanuai kwa kulinda , kusimamia, kuboresha na kukarabati mfumo wa asili wa Maisha zinapaswa kupewa kipaumbele. 

Hali halisi inayoikumba dunia 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji  wa UNEP, Inger Andersen “Ukweli ulio mgumu ni kwamba, mabadiliko ya tabianchi ni juu yetu. Athari zake zitaongezeka na kuzikumba vibaya nchi na jamii zilizo hatarini hata kama tutafikia malengo ya mkataba wa Parisi ya kuhakikisha ongezeko la joto duniani kwa karne hii linasalia chini ya nyuzi joto 2°C na kushusha hadi nyuzi joto 1.5°C. Kama alivyosisitiza Katibu Mkuu tunahitaji ahadi ya kimataifa ya kuweka nusu ya ufadhili wa kimataifa kwa ajili ya mabnadiliko ya tabianchi mwaka ujao katika mikakati ya kuhimili.” 

 Kinachotia moyo katika matokeo ya ripoti hii Bi. Andersen amesema ni kwamba asilimia 72 ya nchi zimepitisha japo kiwango kimoja cha mipango ya kitaifa ya kuhimili janga hilo. 

Nchi nyingi zinaandaa mipango ya kitaifa ya kuhili janga hilo imesema ripoti lakini changamoto ni ufadhili unaohitajika kuitekeleza mipango hiyo haukui haraka inavyotakikana.  

Ingawa unaanza kushika kasi lakini bado unaendelea kuwa mdogo kutokana na ongezeko la kasi za gharama za kuhimili mabadiliko hayo ya tabianchi. 

Kuna matumaini japo kidogo 

Ripoti hiyo imeongeza kuwa tangu mwaka 2006, karibu miradi 400 ya utekelezaji wa mkataba wa Paris inayofadhiliwa na sekta mbalimbali za kimataifa imefanyika katika nchi zinazoendelea. 

Wakatyi miradi ya awali ilikuwa nadra kuzidi dola milioni 10, miradi mipya 21 tangu mwaka 2017 imefikia thamani ya zaidi yad ola milioni 25. 

Hata hivyo ripoti imesema Zaidi ya miradi 1,700 ya kuhimili mabadiliko iliyofanyiwa utafiti ni asilimia 3 pekee ya miradi iliyokwisha tekelezwa ndio tayari imeripoti kupungua kwa hatari zinazoletwa na mabadiliko ya tabianchi . 

Tathimini ya mifuko mmne mikubwa ya kimataifa ya ufadhili dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na maendeleo imesema kiwango cha suluhu za kiasili dhidi ya janga hili kimeongezeka katyika miongo miwili iliyopita. 

Miradi inayofadhiliwa na mifuko hiyo hivi sasa ni ya dola bilioni 94 licha ya hivyo n idola bilioni 12 pekee ndizo zilizotumika katika suluhu za asili. 

Kinachpaswa kufanyika 

Kwa mujibu wa ripoti , kupunguza gesi chafuzi ya viwandani kutapunguza athari nag hara zinazohusiana na mabadiliko ya tabianchi. 

Kufikia lengom la mktaba wa Pasris la nyuzi joto 2°C kutapunguza hasara ya ukuaji wa kila mwaka hadi asilimia 1.6 ikilinganisha na asilimia 2.2 itakayokuwa kutokana na makadirio ya onghezeko la joto ya kufikia nyuzi joto 3°C. 

Ripoti imezitaka nchi zote kutekeleza juhudi zilizoainishwa kwenye ripoti hii ya UNEP ya 2020 ya mapengo ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi ambayo imetoa wito wa dunia kujikwamua katika janga la COVID-19 kwa kuzingatia mazingira lakini pia kuongeza ahadi zao za kitaifa ikiwemo mchango wao wa kutozalisha kabisa hewa ukaa. 

Hata hivyo imesisitiza kwamnba dunia ni lazima iweke mipango ya ufadhili wa kifedha na utekelezaji wa mikakati ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi ili kuzisaidia nchi ambazo hazihusiki sana na kuleta mabadiliko ya tabianchi lakini ndizo zilizo hatarini zaidi.

Audio Credit
FLORA NDUCHA / GRACE KANEIYA
Audio Duration
3'7"
Photo Credit
UNDP