Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni muhimu kuhakikisha shule zinasalia wazi hata wakati wa COVID-19 :UNICEF

Ni muhimu kuhakikisha shule zinasalia wazi hata wakati wa COVID-19 :UNICEF

Watoto hawawezi kumudu mwaka mwingine wa kufurugwa kwa masomo:UNICEF 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema Watoto hawawezi kumudu mwaka mwingine wa masomo yao kuvurugwa huku likitoa wito wa kila juhudi kufanyika kuhakikisha shule zinasalia wazi na kipaumbele kinatolewa kwa zilizofungwa kufunguliwa. Grace Kaneiya na taarifa zaidi 

(TAARIFA YA GRACE KANEIYA) 

Kupitia taarifa yake iliyptolewa leo shirika hilo limesema wakati janga la corona au COVID-19 likiingia mwaka wa pili na idadi ya wagonjwa ikiongezeka kote duniani huu ni wakati wa kuhakikisha mustakbali wa watoto unalindwa na hasa wakiwa shuleni.  

Henrietta Fore mkurugenzi mtendaji wa UNICEF akisistiza hilo amesema “ Licha ya kuwepo na ushahidi mkubwa wa athari za kufunga shule kwa watoto na licha ya ongezeko la ushahidi kwamba shuleni sio kichocheo cha maambukizi ya janga hilo , nchi nyingi zimechagua kuendelea kufunga shule  na zingine kwa karibu mwaka mmoja sasa.” 

Bi Forre amesema gharama za kufunga shule ambapo wakati wa kilele cha maambukizi ya COVID-19 kilichosababisha kila kitu kufungwa na watu kusalia majumbani , asilimia 90 ya wanafunzi waliathirika duniani kote na kuwaacha zaidi ya theluthi moja ya wanafunzi bila fursa ya kusomea majumbani hali ambayo imeleta athari kubwa. 

“Idadi ya Watoto wasiohudhuria masomo inatarajiwa kuongezeka kwa Watoto milioni 24, na kufikia kiwangi ambacho hatujawahi kukishuhudia kwa miaka mingi na ambacho tumepambana sana kutokifikia.” 

 Zaidi yah apo Bi. Fore ameongeza kuwa uwezo wa Watoto kusoma, kuandika na kufanya hisabati za kawaida kabisa umeathirika na ujuzi wanaouhitaji ili kuhimili uchumi wa karne ya 21 umetoweka.  

Hivyo “Afya yao, maendeleo, usalama na ustawi wao uko hatarini na wale walio hatarini Zaidi ndio watakaobeba gharama kubwa. Bila mlo shuleni Watoto wengi walashinda njaa na lishe yao inakuwa duni, bila kucheza na wenzao wanaathirika kisaikolojia na kupata msongo na bila usalama unaopatikana shuleni wengi wako hatarini kufanyiwa ukatili, ndoa za utotoni na ajirija ya watoto.” 

Kwa mantiki hiyo amesisitiza kwamba ndio sababu kufungwa kwa shule inapaswa kuwa suluhisho la mwisho kabisa baada njia zote kufikiriwa kwanza.  

Ametaka endapo kutakuwa nah atua zingine za kufunga kila kitu bai shule zifikiriwe kufunguliwa kwanza kwani “Endapo watoto watakabiliwa na mwaka mwingine wa kufungwa kwa shule athari zake zitadumu kwa vizazi na vizazi vijavyo.” 

Audio Credit
UN News/Grace Kaneiya
Photo Credit
UNICEF/Josue Mulala