Mapambano dhidi ya tabianchi, kijana Nkosi wa Zimbabwe atumia kipaji chake cha kuongea.

Mapambano dhidi ya tabianchi, kijana Nkosi wa Zimbabwe atumia kipaji chake cha kuongea.

Pakua

Nchini Zimbabwe kijana mdogo wa umri wa miaka 17 anatumia kipaji chake cha kuongea kuhamasisha mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Huyo ni Nkosilathi Nyathi mwenye umri wa miaka 17, mkazi wa Victoria Falls, Zimbabwe. Akitumia kipaji chake cha kuzungumza na kughani katika kueneza elimu ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi. 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na mradi wa Fridays for Future ulioanzishwa na vijana ulimwenguni, linawatambua wanaharakati vijana walioko mstari wa mbele katika kupamana na mabadiliko ya tabianchi kama afanyavyo Nkosi. 

Mara nyingi ninasema ninaishi katika mabadikilo ya tabianchi…Ndivyo anavyosema Nkosi. Kwamba marafiki zake wanaishi katika hali hiyo, na familia yake pian a kwamba jambo inabidi lifanyike kuhusu hali hii. 

Anasema anaona mabadiliko kadhaa katika mazingira yake kama vile mawimbi ya joto, mafuriko na ukame. Na anasema anatakiwa kuchukua hatua. 

Kwa kutumia simu yake ya mkononi anaonekana akionesha korongo kubwa na anasema makorongo kama hayo ndiyo yanazidi kusababisha mmonyoko wa udongo hata katika maeneo ya makazi pia. Akieleza pia kuwa watu katika eneo lake wanategemea kilimo na wakati mwingine mvua haziji kwa hivyo wanajikuta kwenye ukame na wakati mwingine wanapata mvua kubwa kuliko kiwango kinachohitajika hivyo anashauri kuwa lazima jambo lifanyike. 

Anasema hakuwa vema sana katika michezo kama wenzake lakini alikuwa mzungumzaji mzuri na alikuwa anashiriki katika mashindano mbalimbali na kwa hivyo ameamua kukitumia kipaji chake hicho kuzungumza kuhusu mabadililko ya tabianchi.  

Anasema changamoto ambayo ameiona ni kuwa baadhi ya vijana hawajui kuhu mabadiliko ya tabianchi, mfano yanavyoendelea katika mazingir yao. Na kwamba wanaona matokeo ya mabadiliko ya tabianchi lakini kimsingi hawajui linaloendelea.  

Ujumbe wa kijana Nkosi ni kuwa hakuna wakati mwingine wa kuchukua hatua kama sasa na kwamba vijana wanapaswa kuwa katika mstari wa mbele kupambania haki ya tabianchi kwani siku za usoni ni zetu.  

 

Audio Credit
Flora Nducha/Ahimidiwe Olotu
Audio Duration
1'6"
Photo Credit
WFP/Matteo Cosorich