Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tenda wema nenda zako, msichana Aneth ambaye kitendo chake kimeendelea kuwasaidia wanafunzi viziwi, Chuo Kikuu cha Dare es Salaam

Tenda wema nenda zako, msichana Aneth ambaye kitendo chake kimeendelea kuwasaidia wanafunzi viziwi, Chuo Kikuu cha Dare es Salaam

Pakua

Katika mahojiano kati ya Ahimidiwe Olotu wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa na Aneth Gerana Isaya, msichana kiziwi ambaye ushauri wake alioutoa alipojiunga katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, umeendelea kuwasaidia viziwi wote wanaojiunga kwa masomo katika Chuo hicho kikongwev cha elimu ya juu nchini Tanzania. Aneth pia ni Mwanzilishi wa shirika la Furaha kwa Wanawake Viziwi Tanzania FUWAVITA. Aneth Isaya anaanza kwa kueleza hatua ambazo wameshapiga katika harakati za kupigania usawa wa kijinsia hususani kwa wanawake wenye ulemavu. Kama nilivyodokeza awali, kwa kuwa msichana huyu anatumia lugha ya ishara, sauti tutakayoisikia hapa ni sauti ya Bwana Billbosco Muna ambaye ni mkalimani Aneth kwa upande wa lugha ya ishara.

Audio Credit
Flora Nducha/ Ahimidiwe Olotu
Sauti
6'51"
Photo Credit
UN Tanzania