Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumepoteza kila kitu:Wakimbizi wa Ethiopia, miaka yote tuliyofanya kazi imepotea bure.  

Tumepoteza kila kitu:Wakimbizi wa Ethiopia, miaka yote tuliyofanya kazi imepotea bure.  

Pakua

Maelfu kwa maelfu ya wakimbizi wa Ethiopia kutoka jimbo la Tigray wanaokimbilia Sudan kunusuru maisha yao, wanapitia madhila mengi ikiwa ni pamoja na kupoteza wapendwa wao na kutojua mustakabali wao limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Jason Nyakundi na maelezo zaidi. 

Kwa mujibu wa shirika hilo wakimbizi hawa wanafunga virago kwa sababu ya machafuko yaliyoanza mapema mwezi huu na kuendelea hadi sasa baina ya serikali kuu ya Ethiopia na vikosi vya jimbo la nchi hiyo laTigray. 

Na ili kuokoa uhai wao wengi wamelazimika kuacha kila kitu na kuondoka mikono mitupu. Miongoni mwao ni mkimbizi Azeeb ambaye amewasili kwenye mji wa mpakani wa Sudan Hamyadet siku tano zilizopita, kwa uchungu mkubwa anasema,“tumefanya kazi kwa miaka mingi Ethiopia na sasa tumeacha kila kitu na kukimbia, tumekuja na nguo tu walizovaaSijui wapi aliko mumwe wangu, nimekuwa nikimtafuta kwa siku tano sasa sijampata na sijui yuko wapi. 

Madhila wanayopitia yalianzia nyumbani Tigray, kama anavyosema mkimbizi Gannite, ingawa hajui machafuko hayo yalivyoanza lakini asilani hatosahau alichokishuhudia, “sijui yalianzaje lakini yalikuwa mapigano makubwa sana na watu wengi wamekufa, baada ya hapo wakatuambia tuondoke, hivyo tukakimbia na kila mtu alikimbia na tukavuka mto Sittet na kufika hapa.” 

Hofu kubwa ya UNHCR hivi sasa ni afya za wakimbizi hawa ambao wamefurika katika kituo kidogo cha mapokezi chenye uwezo wa kuhifadhi watu 300 tu, lakini sasa wanakaribia elfu 20 na idadi ikiendelea kuongezeka huku wakikabiliwa na uhaba wa huduma muhimu ikiwemo chakula, huduma za afya na malazi.. 

Audio Credit
Flora Nducha/Jason Nyakundi
Audio Duration
1'46"
Photo Credit
© UNHCR/Hazim Elhag