Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

18 Septemba 2020

18 Septemba 2020

Pakua

Leo tukimulika mkutano wa 75 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA75 hususan maadhimisho ya miaka 75 ya Umoja wa Mataifa. Mwenyeji wetu leo ni mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Kennedy Gastony.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo amefungua tukio la malengo ya maendeleo endelevu SDG jijini New York Marekani.  Ikiwa leo ni maadhimisho ya kwanza ya siku ya kimataifa ya malipo sawa, muungano wa kimataifa kuhusu malipo sawa, EPIC na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo linalohusika na masuala ya wanawake UN Women na shirika la kazi duniani ILO yametoa wito wa hatua madhubuti kuchukuliwa kutimiza ndoto hiyo ya malipo sawa.  Jitihada zinaendelea nchini Ugiriki ili kuwapa makazi wasaka hifadhi ambao wamepoteza makazi kutokana na moto ambao uliteketeza kituo cha mapokezi na utambuzi cha Moria huko Lesvos. 

 

 

Audio Credit
Flora Nducha\Assumpta Massoi
Audio Duration
12'31"