Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wa Jordan wamenipa fursa nyingine baada ya vita kuniondoa masomoni Yemen-Mkimbizi 

Watu wa Jordan wamenipa fursa nyingine baada ya vita kuniondoa masomoni Yemen-Mkimbizi 

Pakua

Wakiwa katika mavazi ya kazi, vijana wakimbizi wamelizunguka gari na mmoja wao akiwa na kifaa cha kupima gari ili kugundua tatizo.  Ahimidiwe Olotu na taarifa zaidi.

Waleed mwenye umri wa miaka 28, mkimbizi kutoka Sana’a Yemen ni mmoja wa wanaoshiriki masomo ngazi ya astashahada kuhusu ufundi wa mifumo ya kisasa ya magari katika Chuo Kikuu cha ufundi cha Luminus mjini Amman Jordan akiwa na wakimbizi wenzake pamoja na wanafunzi wengine wenyeji raia wa hapohapo Jordan,“nilikuwa najisikia kukata tamaa kwa sababu nilikuwa nimetimiza umri wa miaka 26 hadi 27 na sikuwa nimekamilisha masomo yangu.” 

Waleed aliikimbia nchi yake ya Yemen mwaka 2017 akiwa na kaka, mama na bibi yake na akalazimika kuacha masomo yake ya chuo kikuu wakati huo akiwa katika mwaka wake wa tatu akisomea shahada yaani digrii ya uandishi wa habari,“elimu ni muhimu sana kwa wakimbizi wadogo ili waweze kujitegemea.” 

Duniani kote ikiwa ni asilimia tatu tu ya wakimbizi ambao wanaweza kupata elimu ya juu, Chuo Kikuu cha Ufundi kinatoa mafunzo ya ufundi kwa wakimbizi wakiwa na wenzao wa Jordan n ani moja ya vyuo vichache kutoa fursa sawa za kujifunza kwa raia wakimbizi wenye uraia mbalimbali. Mafunzo yanaanzia kozi fupifupi hadi kufikia miaka mitano ya shahada. Kamishna Mkuu wa UNHCR, Fillipo Grandi anakutana na anafunzi na anasema, “ni mradi ambao una faida nyingi. Kwanza kabisa, unawapa vijana wengi wadogo, raia na wakimbizi, ujuzi wa kupata kazi. Kimsingi, wanawasaidia kupata kazi hizo; wanaoanisha ujuzi na fursa za ajira. Lakini pia ni zana muhimu ambayo kwayo, wakimbizi na nchi ya Jordan ni moja ya nchi zinazohifadhi wakimbizi wengi duniani, wanaweza kujumuishwa katika uchumi kipindi ambacho wanalazimika kuishi mbali na nyumbani kwao.” 

Hivi sasa, karibu wanafunzi 1,800 wakimbizi wameandikishwa katika shule hiyo. UNHCR inasaidia ufadhili wa wakimbizi 29 wa mataifa tofauti na 29 wa Jordan. 

Audio Credit
Flora Nducha/Ahimidiwe Olotu
Audio Duration
1'54"
Photo Credit
UN News