Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

15 Septemba 2020

15 Septemba 2020

Pakua

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya demokrasia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema demokrasia ni muhimu katika kuhakikisha upatikanaji wa taarifa, ushiriki katika ufanyaji maamuzi na uwajibikaji wa kuchukua hatua hasa wakati huu ambapo dunia inakabiliana na janga la corona au COVID-19. Mashirika ya Umoja wa Mataifa yametoa mwongozo wenye mapendekezo ya mikakati ya kiafya ya kuzingatiwa na serikali kuhusu linin a jinsi ya kufungua tena shule kwenye maeneo ambako shule bado zimefungwa kutokana na janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19.Hatimaye mamia ya wasaka hifadhi kwenye kambi ya Moria iliyoteketetea kwa moto katika kisiwa cha Lesvos nchini Ugiriki wiki iliyopita, sasa wamepata makazi kwenye mahema yaliyosimikwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
12'25"