Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zambia, UNICEF yasaidia wanaokabiliwa na uhaba wa maji

Zambia, UNICEF yasaidia wanaokabiliwa na uhaba wa maji

Pakua

Nchini Zambia, mradi wa maji uliofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, umekuwa nuru kwa wakazi 800,000 wa wilaya ya Gwembe kusini mwa Zambia.  Ahimidiwe Olotu na maelezo zaidi.

Katika wilaya ya Gwembe mtoto Sandra na baba yake Stanford Hangoma wanafukuza ndege kutoka kwenye shamba lao wakati huu ambao inaelezwa kuwa zaidi ya wananchi milioni 2.3 wanakabiliwa na athari za ukame nchini Zambia.
Stanford anakiri kuwa wamekuwa na vipindi vya ukame kwa miaka mitatu iliyopita na sasa 2020, mazai hayakuota na kwamba yote yalipotea.
UNICEF inasema kuwa Zambia ni miongoni mwa nchi 9 za kusini mwa Afrika zilizokumbwa na janga la dharura kwenye suala la uhakika wa chakula.
Familia zinakumbwa na mazingira magumu na ya ukweli kuhusu COVID-19 na msaada wa kila mwaka unayoyoma ambapo Stanford anasema kuwa, “Watoto wengi hawawezi kwenda shuleni kwa sababu ya njaa, utapiamlo, na kwa ujumla watoto wengi hawaendi shuleni. Kwa ujumla watoto hawako shuleni kwa sababu ya kusaka maji.”

Samson Muradzikwa ni Mkuu wa será na utafiti UNICEF nchini Zambia akisema kuwa, “watoto wengi hawakuweza kwenda shule kwa sababu ya njaa. Kiwango kikubwa cha utapiamlo na unyafuzi na kwa ujumla, watoto wengi wasio na huduma za maji watakwenda kusaka maji.”
Hadi sasa, wakazi wa Ngwede wamenufaika na ufungwaji  wa pampu 60 ambapo Maureen anasema ni jambo jema na kwamba, “Tulifurahi sana pindi pampu ya maji ilipofungwa. Tulikuwa tunatembea mbali kushuka vilima ili kuteka maji na unapanda mlima ukiwa umebeba maji. Ulikuwa mzito tosha! Sasa tuna furaha tuna maji.”
Kwa Sandra sasa anaendelea na shule, na ingawa wazazi wake hawawezi kumnunulia sare mpya za shule, angalau ana muda mwingi wa kucheza badala ya kwenda kuteka maji umbali mrefu na hata akisema, “nataka kurejea shule na niwe muuguzi.”

Audio Credit
Assumpta Massoi/Ahimidiwe Olotu
Audio Duration
1'33"
Photo Credit
© UNICEF/Shehzad Noorani