Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kama nzige hawa hawataisha na mvua ikanyesha japo kiasi, mifugo yetu itakufa- Wafugaji Turkana

Kama nzige hawa hawataisha na mvua ikanyesha japo kiasi, mifugo yetu itakufa- Wafugaji Turkana

Pakua

Hivi karibuni tulikueleza namna ambavyo nzige wavamizi wa jangwani wanavyotishia ustawi wa wakulima wa Kenya hususani eneo katka eneo la Turkana, lakini kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo la Umoja wa mataifa FAO, nzige hao hawaishii tu katika kilimo bali pia wanatishia jamii ya wafugaji kwani wanakula hadi nyasi na miti amayo ingekuwa chakula cha kifugo. John Kibego na maelezo zaidi. 

Maisha ya wakulima wafugaji katika Kaunti ya Turkana nchini Kenya yameathiriwa sana na uvamizi unaoendelea wa nzige wa jangwani ambapo asilimia ishirini ya mazao yameharibiwa katika maeneo ambayo wadudu wameonekana.  Wafugaji wanasema hali imekuwa mbaya kwa malisho kiasi kwamba hivi sasa hata mifugo haitoi maziwa ya kutosha kama ilivyokuwa awali na hivyo wanalazimika kuongeza maji kwenye maziwa ili angalau yaweze kuwatosha watoto wao. 

Wafugaji wana wasiwasi kuwa hakutakuwa na chakula cha kutosha kwa ajili ya mifugo yao kwani pamoja na uwepo wa nzige, msimu wa ukame unakaribia. Moses Areng ni mmoja wa wafugaji anasema, “Sijui kwa nini nzige wa jangwani walikuja, Mungu pekee anafahamu. Kama wangalikuwa wanaongea wangwtuambia wao ni waturkana kwasababu wamezaliwa hapa hawana pa kwenda, kumaanisha wangeendelea kuishi na kuzaliana hapa.” 

Kutokana na hali hii ya sintofahamu inayosababishwa na wadudu hawa waharibifu, Moses Areng, ana mashaka na mstakabali wa jamii yake ya wafugaji ambao ni wakulima pia. “Ikiwa nzige watatoweka sasa, na ikiwa Mungu atatupatia mvua kiasi, tunafahamu kuwa mifugo wataongezeka. Lakini kama mvua haitanyesha kwa zaidi ya mwezi mmoja na makundi ya nzige yakamaliza malisho yaliyopo, ng’ombe wetu watapungua na kufa kwa njaa na magonjwa.” 

Silali Turkwell ni Afisa kilimo wa Turkana anasema, “Kwa watu hawa, madhara ambayo yametengenezwa na Nzige ni ukosefu wa uhakika wa chakula. Baada ya kumaliza mazao watakula malisho ya mifugo na miti. Na ikiwa wataenda kwenye miti ni ukosefu wa uhakika wa chakula kwa binadamu na mifugo. Na ikiwa mifugo itaondoka, kinachofuata ni binadamu watakaoondoka.” 

Tangu mwanzoni mwa mwezi Januari hadi mwezi huu wa Agosti, zaidi ya hekari 600,000 zimeokolewa kote katika ukanda wa Afrika Mashariki. Kwa makadirio ya FAO, hadi kufikia sasa, zaidi ya nusi trilioni ya nzige wameuawa katika eneo lote la Afrika Mashiriki lakini tishio la uwezekano wa kuzaliana tena bado lipo kuelekea mwishoni mwa mwaka hu una kwa hivyo vita dhidi ya wadudu hawa waharibifu inapaswa kuendelea.  

Audio Credit
Flora Nducha\John Kibego
Audio Duration
2'50"
Photo Credit
WFP/Peter Louis