Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa una fursa nyingi, muhimu vijana tuwe tayari na tuwe na moyo wa kujitolea-Hilda Phoya

Umoja wa Mataifa una fursa nyingi, muhimu vijana tuwe tayari na tuwe na moyo wa kujitolea-Hilda Phoya

Pakua

“Umoja wa Mataifa una fursa nyingi ambazo ikiwa vijana tutakuwa na moyo wa kujitolea na bidii ya kazi, tunaweza kunufaika nazo,” hayo ni maoni ya Hilda Phoya, mwanafunzi ambaye hivi karibuni amehitimisha mafunzo kwa vitendo katika Kituo cha habari za Umoja wa Mataifa UNIC Dar es Salaam Tanzania. 

Katika mahojiano haya yaliyofanywa na Ahimidiwe Olotu wa Kituo hicho, Hilda anaanza kwa kueleza kilichomvutia kuchagua kwenda katika kituo hicho ili kukamilisha masomo yake ya elimu ya juu. 

Kitu ambacho nilinivutia kuja hapa au kutuma maombi yangu hapa ni nafasi ambayo Umoja wa Mataifa inakupa sio tu nchini lakini pia duniani kwa ujumla,niliona nidhahiri kwangu kujifunza hasa kwa vitendo kile ambacho nimesoma darasani nimejifunza mengi kwa kuanza nimechukua video nilikuwa sifahamu lakini pia nimejifunza kazi mbalimbali kama kituo chetu cha habari kina maktaba kwa hivyo kazi za maktaba pia nimejifunza kazi zingine za ofisi zinazohusiana na maswala ya habari na taarifa lakini pia habari nimejifunza na pia nimejifunza kwa ndani zaidi maswala ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs na pia nimepata nafasi ya kutembelea shule mbalimbali nikiwa hapa kituo hiki cha habari cha Umoja wa Mataifa. Kuweza kuzungumza na wanafunzi juu ya mambo mengi na hayo pia yamenijenga mimi kwa namna moja au nyingine katika kipindi hiki ambapo nilikuwa nafanya mafunzo yangu hapa

Kuhusu wito wake kwa Umoja wa Mataifa katika kuendelea kuwapa nafasi vijana hususana wasichana, Hilda anasema,

Ni jambo njema na ni jambo nzuri kwa Umoja wa Mataifa kwendelea kutoa nafasi hizi kwa wanafunzi hasa wasichana ili waweze kuwasaidia ama kutusaidia mimi nikiwa mmoja wapo kuweza kutusaidia kuingia na kufanya kazi

Na je, Hilda ana ushauri gani kwa vijana wenzake?

Tuwe na moyo wa kujitolea tuwe na utayari na nidhamu ya kujitolea na kufanya kazi kwa bidii tuwe tayari kwa sababu kama Umoja wa Mataifa inanafasi nyingi ambazo inatoa sio tu katika kituo cha habari lakini pia katika mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa kuna nafasi nyingi za vijana kujitolea kwa hivyo tuwe na utayari na nidhamu ya kujitolea. Nashukuru kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa Tanzania,nashukuru Umoja wa Mataifa wote kwa ujumla na wale ambao tumefanya kazi pamoja wamekuwa msaada mzuri kwangu na wamenisaidia kwa kweli na popote ambapo nitaenda nitakumbuka mafunzo na nitaendelea kutia juhudi nitawakilisha vyema Umoja wa Mataifa kwa nafasi yangu mimi ya kuwa hapa. 

Audio Credit
Anold Kayanda\Ahimidiwe Olotu
Audio Duration
3'7"
Photo Credit
UN News/Elizabeth Scaffidi