Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

14 Agosti 2020

14 Agosti 2020

Pakua
Jaridani la Umoja wa Mataifa Ijumaa ya leo na Assumpta Massoi
- Leo kenye mada yetu kwa kina  tunaangazia harakati za vijana katika kulifikia lengo namba 16 la maendeleo endelevu, SDG ambalo linapigia chepuo masuala ya haki, utawala bora na taasisi thabiti.
-Leo Agosti 14, imetimia miezi sita tangu kuthibitika kwa mgonjwa wakwanza wa COVID-19 barani Afrika. T
- Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limesema kwa kushirikiana na serikali ya Kenya wamepiga hatua kubwa kudhibiti nzige waliovamia kaunti 29 mwezi Februari mwaka huu na sasa ni kauanti chache tu ikiwemo Turkana ambazo bado zina tatizo.
-Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP  limesema Watu wanne kati ya kumi wako katika hali ya kukosa chakula nchini DRC na msaada zaidi unahitajika
-Na katika kujifunza kiswahili leo tunakwenda Kenya kwa uchambuzi wa methali na mtaalam wetu  ni Josephat Gitonga, mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi katika kituo cha tafsiri na ukalimani  ambapo leo tutajifunza maana ya methali "HERI KENDA MKONONI KULIKO KUMI NENDA RUDI" Karibu!

 

 
Audio Credit
Assumpta Massoi
Sauti
11'52"