Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

07 Agosti 2020

07 Agosti 2020

Pakua

Jaridani la Umoja wa Mataifa hii leo na Assumpta Massoi 
- Leo ikiwa ni Ijumaa ni mada kwa kina ambapo tutamulika unyonyeshaji wa mtoto maziwa ya mama kwa kuzingatia kuwa tuko
katika wiki ya unyonyeshaji duniani
 - Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na wadau wanaharakisha hatua za kusaidia serikali ya Lebanon baada ya mlipuko wa jumanne huko Beiruti.
- Mashirika ya Umoja wa Mataifa  IOM na UNHCR, wamehuzunishwa na vifo vya watu 27 vilivyotokea baada ya boti walimokuwa wakisafiria kuzama karibu na pwani ya Afrika Magharibi.
 -Na kuelekea siku ya watu wa jamii ya asili keshokutwa jumapili ya tarehe 9 mwezi huu wa Agosti, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kuna umuhimu wa kutambua haki za watu wa asili na kuwajumuisha katika mapambano dhidi ya COVID-19.
 -Na leo kwenye neno tunaenda Uganda kwa  Mwenyekiti wa idara za Kiswahili katika vyuo vikuu Afrika Mashariki Aida Mutenyo kufafanua maana ya methali "Adhabu ya kaburi aijuaye Maiti" Karibu 

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
9'51"