Jaridani la Umoja wa Mataifa hii leo na Assumpta Massoi
- Shirika la mpango wa chakula duniani
WFP wajitosa kuisaidia Lebanon kwani bila bandari ya Beirut, hali itakuwa mbaya zaidi Lebanon
- Wanawake wafungwa katika gereza la Bimbo wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, Bangui watanufaika na mradi wa ujumuishwaji katika jamii unaotekelezwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini humo,
MINUSCA.
-Na leo kwenye Makala tunakwenda Uganda ambako kilimo cha pilipili kimegeuka lulu kwa mstaafu ambaye awali alilima zaidi mahindi na maharage.
-Na kwenye mashinani leo tunakwenda Burundi kusikia jinsi shirika la Cartedo linajengea uwezo vijana kuhimili maisha hata wakati wa majanga, Karibu!