Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sikiliza jinsi raia wa Kenya alivyonasuliwa kwenye zahma ya usafirishaji haramu

Sikiliza jinsi raia wa Kenya alivyonasuliwa kwenye zahma ya usafirishaji haramu

Pakua

Na sasa ni wasaa wa mada yetu kwa kina ambayo leo inaangazia usafirishaji haramu wa binadamu na changamoto zake. Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na madawa na uhalifu UNODC inasema hili ni tatizo mtambuka linaloikumba dunia nzima na linalohitaji jududi za pamoja za kimataifa kupambana nalo. Kwa mujibu wa takwimu za ofisi hiyo watu milioni 40 kote duniani wamekwama katika janga la  usafirishwaji haramu wa binadamu huku waathirika wakubwa wakiwa ni wanawake na wasicha takribani asilimia 70, ambao wengi huingizwa katika biashara ya ukahaba, kutumikishwa kama watumwa majumbani, mashambani na katika kazi nyingine ngumu kwa ujira mdogo na wakati mwingine bila malipo yoyote. Mwandishi wetu wa Nairobi Jason Nyakundi amezungumza na mmoja wa waathirika Rachel Olusa ambaye kwa msaada wa polisi alifanikiwa kuponyoka na kurudi nyumbani Kenya na pia mwanaharakati wa kupigania masuala ya wanawake na haki za binadamu Ruth Mumbi. Kwako Jason . 

Audio Credit
Assumpta massoi/Jason Nyakundi
Audio Duration
5'55"
Photo Credit
UNODC