Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nilijifunza mtandaoni kutengeneza viungo vya chai kisha nikaboresha ujuzi SIDO- Emma Zibiliza 

Nilijifunza mtandaoni kutengeneza viungo vya chai kisha nikaboresha ujuzi SIDO- Emma Zibiliza 

Pakua

Emma Zibiliza ni kijana msomi nchini Tanzania ambaye amesukumwa na mambo mawili ya msingi kuingia katika ujasiriamali. Kwanza ni kupambana na hali ya ukosefu wa ajira iliyoko duniani, ambapo kwa hili analenga kujikwamua, kuwakwamua vijana wenzake kwa kuwaajiri, na pia kuwapa kipato wakulima wa malighafi anazozitumia katika mradi wake mpya wa kusindika mazao ili kutengeneza viungo vya chai. Kutokana na ujuzi alioupata mitandaoni na kisha ujuzi huo ukanolewa na shirika linalosimamia viwanda vidogo nchini Tanzania, SIDO, Emma Zibiliza amefanikiwa kuingiza sokoni bidhaa zake mbalimbali za viungo vya chai vinavyotumia mazao ya asili, jambo ambalo ndilo msukumo wake, kuona jamii ikitumia bidhaa zisizo na kemikali. Kutoka Dar es Salaam, Hilda Phoya wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, ameandaa makala ifuatayo kumuhusu mjasiriamali huyu. 

Audio Credit
Anold Kayanda/Hilda Phoya
Audio Duration
4'3"
Photo Credit
UN/Emma Zibiliza