Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkimbizi nchini Uganda aeleza alivyopata moyo wa kulea mtoto aliyekimbia bila wazazi.

Mkimbizi nchini Uganda aeleza alivyopata moyo wa kulea mtoto aliyekimbia bila wazazi.

Pakua
Kutokana na mizozo ya bunduki maelfu ya watoto hulazimika kukimbia nchini mwao bila kusindikizwa na wazazi au mtu mzima yeyote na kujikuta katika nchi jirani. Mara nyingine hujikuta mikononi mwa wanaowafanyia ukatili wa aina mbalimbali ikiwemo ukatili wa kingono kwa watoto wa kike chini ya mwavuli wa kuwalea. Kulingana na ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR ya mwezi Machi mwaka huu 2020, Uganda ilikuwa na watoto elfu arubaini na mmoja na arubaini na mmoja 41,041 waliokimbia bila wazazi au kutenganishwa na familia zao.
Hata hivyo wakimbizi wenzao hujitahidi kwa kushirikiana na UNHCR kuona kwamba watoto hawa wanapata ulinzi sitahiki na kukuzwa kitamaduni katika mpangilio wa familia za kiafrika. Je,wanapata wapi moyo wa kujitolea kulea watoto hawa? Katika kambi ya wakimbizi ya Kyangwali, John Kibego amezungumza na Shantale Munyandinda mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia kongo, DRC, mmoja wa wanawake ambao wamejitolea kutoa malezi kwa watoto zaidi za 2,500 waliokimbia mizozo bila kusindikizwa na watu wazima.
Audio Credit
Loise Wairimu\ John Kibego
Audio Duration
4'2"
Photo Credit
OCHA/Steve Hafez