Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

29 JULAI 2020

29 JULAI 2020

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema kuwa nyongeza ya watoto milioni 6.7 wenye umri wa chini ya miaka mitano wanaweza kupata tatizo la kuwa na uzito mdogo zaidi kulingana na urefu wao na hivyo kuwa na unyafuzi kutokana na madhara ya kiuchumi na kijamii yatokanayo na janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19. Luteni Kanali John Ndunguru, Kamanda wa kikundi cha 7 cha Tanzania, TANZBATT 7, kwenye kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO anaelezea mpangilio wa ratiba yake kwa siku. Ikiwa ni sehemu ya msaada wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO kwa harakati za Azerbaijan kupambana na virusi vya corona au COVID-19, mradi wa REACT-C19 umewaleta madaktari 19 raia wa Azerbaijan waliokuwa wanafanya kazi Uturuki ili warudi nyumbani kusaidia kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa sekta ya afya kuhusu jinsi ya kushughulikia COVID-19.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
12'34"