Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wachimba chumvi waomba msaada, walalamikia vikwazo vya kuzuia COVID-19, Uganda

Wanawake wachimba chumvi waomba msaada, walalamikia vikwazo vya kuzuia COVID-19, Uganda

Pakua

Nchini Uganda,katika eneo la magharibi mwa nchi hiyo kandoni mwa ziwa Albert, wanawake wa eneo hilo wanaoegemea biashara ya uchimbaji na uuzaji chumvi maarufu kwa jina la chumvi ya Kibiro ambayo pamoja na matumizi ya kawaida ya mapishi hutumika pia katika dawa za asili wamejikuta katika wakati mgumu kwani ufikiaji wa maeneo ya ziwani umekubwa na changamoto lukuki ambazo ni pamoja na vikwazo vya usafiri vilivyowekwa na serikali ili kudhibiti kuenea kwa COVID-19, pia mafuriko yaliyoziba mtandao wa barabara, kufungwa kwa masoko, kufurushwa baadhi ya wakazi wa Ziwa Albert kwenye mialo iliobainishwa na serikali kuwa ni makazi haramu. Mwandishi wetu wa Uganda ametembelea maeneo hayo na kututumia makala hii. 

 

Audio Credit
Anold Kayanda/John Kibego
Audio Duration
4'
Photo Credit
UN/ John Kibego