Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

21 JULAI 2020

21 JULAI 2020

Pakua

Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

- Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO limetoa ripoti mpya ya tathimini ya misitu duniani ikionyesha kwamba misitu inaendelea kupotea kutokana na matumizi mbalimbali ikiwemo kilimo na upanuzi wa makazi hasa barani Afrika

-Vijana watatu nchini Tanzania wamebuni mfumo wa kuweka umeme kwenye mita kwa njia ya simu ambao utawasahisishia wateja wa huduma hiyo muhimu

-Mradi wa pamoja wa Kigoma, KJP nchini Tanzania unaoendeshwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa umeendelea kuwa baraka kwa wakazi wa mkoa huo ambapo wanufaika wa hivi karibuni zaidi ni kikundi cha wanawake kata ya Janda wilaya ya Buhigwe 

-Makala yetu leo inatupeleka Magharibi mwa Uganda kumulika wanawake wachimbaji wa chumvi

-Na mashinani tuko kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS utamsikia mmoja wa walinda amani kutoka Ethiopia akizungumzia doroa na changamoto zake

Audio Credit
UN News Flora/Nducha
Audio Duration
11'24"