Jaridani la Umoja wa Mataifa hii leo.
- Shirika la afya ya wanyama duniani OIE na shrika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO leo wamezindua mkakati wa pamoja wa hatua za kimataifa za kuzuia kusambaa kwa homa ya mafua ya nguruwe ya Afrika
- Mkimbizi raia wa Syria ambaye hivi sasa anaishi Ufaransa, amejizolea sifa kwa kuandaa chakula kwa ajili ya kuwasambazia wafanyakazi walioko katika mstari wa mbele wa kupambana na janga la COVID-19 katika nchi yake mpya.
- Sintosahau nilichokishuhudia kambini Bangladesh:Mkimbizi Asma
-Kwenye makala leo tutakwenda pwani mwa Kenya kuangazia hofu ya wakazi wa eneo hilo kuhusu uharibifu wa mazingira. .
-Na leo kwenye mashinani leo tunakwenda Somalia kusikia jinsi Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP linasaidia katika kutoa msaada kwenye kituo cha afya cha kupiga simu zinazo husiana na COVID-19