26 JUNI 2020

26 Juni 2020

Leo hii katika jarida la mada kwa kila la Umoja wa Msataifa Flora Nducha anakuletea

-Ikiwa leo ni siku ya kupinga matumizi ya madawa ya kulevya, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesisitiza kauli mbiu ya mwaka huu inayolenga uelewa mzuri ili kuhakikisha huduma bora kutokana na taarifa sahihi na uwajibikaji wa pamoja katika kupambana na madawa ya kulevya na athari zake 

-Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF katika ripoti yake iliyotolewa leo limesema licha ya changamoto lukuki limefanikiwa kufikisha msaada kwa nchi zaidi ya 100 kupambana na janga la corona au COVID-19 na kuokoa maisha ya mamilioni ya watu. 

-Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, ili kusaidia kuwakinga watu dhidi ya COVID-19, umeunganisha nguvu na Kanisa Katoliki jimbo la Yambio-Tambura kusambaza barakoa zilizotengengenezwa kienyeji kwa jamii za maeneo hayo. 

-Mada yetu kwa kila leo imejikita Tanzania katika sobber house kuzungumza na manusura wa dawa za kuleya , mwanzilishi wa kituo hicho na shughuli wanazozifanya vijana baada ya kuacha dawa za kulevya

-Na katika kujifunza Kiswahili ada ya kila Ijumaa leo Dkt. Mwanahija ali Juma kutoka BAKIZA anatufafanulia maana ya neno  "TOBO"

 

Audio Credit:
UN News/Flora Nducha
Audio Duration:
10'47"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud