Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulinzi wa amani na michezo wadhihirika huko Mavivi, DRC

Ulinzi wa amani na michezo wadhihirika huko Mavivi, DRC

Pakua

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, walinda amani kutoka Tanzania wanaohudumu katika kikosi cha 7 cha nchi hiyo, TANZBATT 7, cha kujibu mashambulizi, FIB, cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO wamepanua wigo wa ukarimu wao kwa watoto na vijana wa eneo la Mavivi, mjini Beni jimboni Kivu Kaskazini.  Luteni Issa Mwakalambo wa TANZBATT 7 na maelezo zaidi.

Walinda amani wa Tanzania nchini DR Congo wakiongozwa na mkuu wa kikosi Luteni Kanali John Ndunguru wakiwa katika mazoezi ya kawaida eneo la mavivi jimboni Kivu Kaskazini. Katika msafara wao wanakutana na watoto na fikra za usaidizi zikawajia kama anavyoelezea Luteni Kanali Ndunguru.

“Tukiwa katika matukio yetu ya ulinzi wa amani tunashirikiana na jamii inayotuzunguka pamoja na majukumu yetu ya msingi pia tunadumisha mahusiano na jamii inayotuzunguka ikiwa ni sehemu mojawapo ya majukumu yetu.Tukiwa katika mazoezi yetu ya kawaida tulikuta jamii ikiwa na mahitaji hayo ya michezo kwa hivyo tuliona ni vizuri tukachangie tunavyoweza kuchangia ili waweze kudumisha michezo ikiwa ni sehemu ya kutengeneza afya zao.”

Lakini je viongozi wa eneo hili wanasemaje? Chifu Makofi anafunguka?

“Kitu cha kwanza ni kumshukuru Kamanda wa kikosi kwa tendo zuri kubwa analofanya kwa watoto wetu ya pili pia nashukuru umoja unaokuwa katikati yetu sisi raia wa DRC katika mji wa Mavivi na watanzania kwa jumla kwasababu ulinzi tunaopata leo unafanya mwaka mzima tunakuwa na usalama tangu tarehe 13 mwezi wa Mei mwaka wa 2019 hadi tarehe 13 mwezi wa Mei mwaka wa 2020 tumefanya mwaka mzima wa usalama kufuatana na ulinzi tunaopewa na watanzania FIB na Jeshi letu hilo. Tendo kubwa linalooneshwa leo ni moja kati ya shukrani tunaweza endelea kufanya kwasababu watoto wataendelea kuwa na kumbukumbu ya tendo la leo kwasababu itakuwa ni kumbukumbu ya siku ya usalama kwetu Mavivi zaidi ya mwaka mmoja kwa hivyo ni siku kubwa kwetu ya kupokea tena kamanda wa kikosi kwa kuja kuwapongeza watoto kwa kutufurahisha kwa mchezo wa kandanda.Tunasema kwa niaba ya Chofu wa kiasili tunashukuru sana kwa tendo kubwa kama hili.”

Jacques Manuku ,Chifu wa Kata ya Matembo akaenda mbali zaidi akisema kuwa,

“Inaweza kutusaidia kwa sababu masomo hayapo kutokana na ugonjwa wa corona na watoto watakuwa wanacheza mpira ambao pia utakuwa unatusaidia sisi wazazi.”

Audio Credit
Anold Kayanda/Issa Mwakalambo
Audio Duration
3'19"
Photo Credit
UN