Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ingawa dunia ina chakula cha ziada watu milioni 830 wanakabiliwa na njaa:UN

Ingawa dunia ina chakula cha ziada watu milioni 830 wanakabiliwa na njaa:UN

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema dunia ina chakula cha kutosha kulisha watu wote na ziada lakini cha kusikitisha ni kwamba watu zaidi ya milioni 800 wanakabiliwa na njaa. Jason Nyakundi anafafanua zaidi.

Bwana Guterres ameyasema hayo leo kupitia ujumbe maalum wa uzinduzi wa sera kuhusu uhakika wa chakula uliofanyika kwa njia ya mtandao na kusema kuwa kuna zaidi ya chakula cha kutosha ulimwenguni kulisha idadi yote ya watu bilioni 7.8 lakini

“Leo hii, zaidi ya watu milioni 820 wana njaa. Na watoto wapatao milioni 144 wa chini ya umri wa miaka 5 wamedumaa , ikiwa ni zaidi ya mtoto mmoja kati ya watoto watano duniani. Mifumo yetu ya chakula inashindwa, na janga la Covid-19 linafanya mambo kuwa mabaya zaidi.”

Ameonya kwamba endapo hatua za haraka hazitachukuliwa, ni dhahiri kwamba kuna dharura ya chakula ulimwenguni ambayo inaweza kuwa na athari za muda mrefu kwa mamia ya mamilioni ya watoto na watu wazima.

Ameongeza kuwa

“Mwaka huu, watu milioni 49 zaidi wanaweza kutumbukia katika umaskini uliokithiri kwa sababu ya janga la Covid-19. Idadi ya watu watakao kuwa na upungufu wa chakula au ukosefu wa lishe bora itaongezeka haraka. Na kila kiwango cha asilimia kinachoshuka katika jumla ya pato la taifa inamaanisha watoto milioni 0.7 zaidi watadumaa.”

Guterres amesem leo  anazindua mpango wa sera wa athari za COVID-19 katika uhakika wa chakula na lishe. Ambayo ina matokeo matatu ya wazi.

“Kwanza, lazima kuhamasisha kuokoa maisha na uhai, kwa kuzingatia umakini ambapo hatari ni kubwa sana, Pili, lazima kuimarisha mifumo ya kuilinda jamii kwa ajili ya lishe na tatu, lazima tuwekeze kwa ajili ya baadaye.

Amehitimisha akisema “endapo tutafanya mambo haya na zaidi, kama tunavyozindua leo, tunaweza kuzuia athari mbaya zaidi za janga la COVID-19 katika uhakika wa chakula na lishe na tunaweza kufanya hivyo kwa njia inayounga mkono mabadiliko ynayojali mazingira ambayo tunahitaji kuyatengeneza.”

 

Audio Duration
2'18"
Photo Credit
UNDP