Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kinga dhidi ya COVID-19 yaleta fursa ya kipato kwa mwanamke mjasiriamali, Uganda

Kinga dhidi ya COVID-19 yaleta fursa ya kipato kwa mwanamke mjasiriamali, Uganda

Pakua

Mlipuko wa virusi vya corona duniani umekwamisha uchumi wa mataifa mengi na vyanzo vya mapato kwa watu wa karibu tabaka zote. Hata hivyo wale ambao wameweza kupunguza athari za maradhi haya kiuchumi ni wajasiriamali wabunifu wanaobadilika na mazingira yaliyopo. Nchini Uganda mwanamke fundi cherehani ambaye pia ni mkufunzi wa wanawake wenzake kufanya kazi hiyo kando na kumiliki duka la nguo, amefanikiwa kudhibiti athari za mlipuko wa virusi vya corona kwa kujikita katika ushonaji wa barakoa akiwa nyumbani kwake wakati wa agizo la kufungwa kwa maduka yote yasio ya chakula.  Hii ni kwa kutambua fursa katika agizo la rais la kuwataka mwananchi wote kuvaa barakoa kama mojawapo ya njia za kuzuia kuenea kwa virusi vya corona. Hii hapa maelezo zaidi katika mahojiano kati ya mjasiariamali Catherine Tibagwa na Mwandishi wetu wa Uganda, John Kibego akiwa katika vitongoji vya mji wa Hoima anaeleza zaidi katika mahojiano haya na mjasiriamali Catherine Tibagwa.

 

Audio Duration
4'1"
Photo Credit
World Bank/Sambrian Mbaabu