Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikundi cha Umoja ni Nguvu Kakonko chanufaika na mafunzo ya FAO

Kikundi cha Umoja ni Nguvu Kakonko chanufaika na mafunzo ya FAO

Pakua

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania wamesaidia wakulima hususan wilayani Kakonko  mkoani Kigoma kupata mbinu bora za kilimo na kuondokana na kilimo cha mazoea na hatimaye waongeze mazao ili siyo tu kukabiliana na umaskini bali pia kutokomeza njaa. Assumpta Massoi hivi karibuni alitembelea mkoa wa Kigoma na kuandaa taarifa ifuatayo.

Katika kata ya Katanga, wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma, wanawake wa kikundi cha Umoja ni nguvu, wanapalilia shamba lao nyakati za asubuhi wakiwa na ari kubwa.

Wengine wanamwaga mbolea kwenye shamba hili la mahindi na maharagwe.

Shamba hili darasa ni matokeo ya mafunzo yaliyotolewa na FAO kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania. Salvasia Silivesta Barumbwa ni kiongozi wa kikundi hiki chenye wanachama 39.

Je kanuni za kilimo bora zinafuatwa? Masumbuko William Masolwa ni Afisa kilimo,kata ya Katanga..

Paskazia Kazibwa ni mkulima mwezeshaji wa kikundi na nilimuuliza nini kinawatia hamasa?

Na ujumbe wake kwa wanawake wengine ni upi?

Mradi umefikisha matokeo chanya hata kwa watoto wao, Paskazia ni shuhuda..

Tayari mahindi na maharagwe yameshavunwa na wakulima wanajiandaa kwa msimu ujao.

Audio Credit
Anold Kayanda/Assumpta Massoi
Sauti
2'52"
Photo Credit
FAO Tanzania