Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunahimiza watu wengi zaidi kuwekeza katika nyuki ili kulinda mazingira na nyuki wenyewe   

Tunahimiza watu wengi zaidi kuwekeza katika nyuki ili kulinda mazingira na nyuki wenyewe   

Pakua

Kila tarehe 20 ya mwezi Mei ulimwengu unaazimisha siku ya nyuki duniani ili kukuza uelewa kuhusu umuhimu wa wadudu hawa ambao wanasaidia katika ustawi wa dunia.  Hata hivyo kutokana na shughuli za binadamu, nyuki wanazidi kuwa hatarini japokuwa ni wazi kuwa mchango wao katika uchafushaji wa mimea ni muhimu kwa mstakabali wa ustawi na uwepo wa dunia. Katika kuliona hilo, vijana mkoani Mwanza nchini Tanzania wameanzisha karakana ya kutengeneza mizinga ya kisasa ili kuwanusuru wadudu hao muhimu ikiwa ni pamoja na kujipatia faida nyingine kama asali na kipato. Hilda Phoya wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC Dar es salaam, anamuhoji msimamizi wa karakana hiyo. 

 

Audio Credit
Loise Wairimu/Hilda Phoya
Audio Duration
3'23"
Photo Credit
UNDP Moldova