Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchini Kenya, Wafransisko Wakapuchini washiriki kutunza mazingira

Nchini Kenya, Wafransisko Wakapuchini washiriki kutunza mazingira

Pakua

Utunzi wa mazingira ni moja ya malengo makuu ya Umoja wa Mataifa.

Lakini dini inachukua nafasi gani katika kuwashauri waumini kuwa katika mstari wa mbele katika utunzaji wa mazingira. Shirika la Wafransisko Wakapuchini  ambalo liko chini ya kanisa na katoliki ni moja ya mashirika ambayo yako katika mstari wa mbele kutunza mazingira kwa ushirkiano na shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP.  Mwandishi wa Nairobi, nchini Kenya, Jason Nyakundi alihudhuria sherehe za kanisa hilo zilizofanyika Nairobi na kuzungumza na Brother Benedict Ayodi, ambaye pia ni Mkurugenzi wa vuguvugu la mazingira la kanisa katoliki barani Afrika.

Sherehe ya leo ni kama kuweka ishara ya kuonyesha kwamba tumemaliza miaka mitano tangu baba Mtakatifu atoe barua yake ya Udatusi  na pia ni kuwahimiza hasa zaidi ndugu na dada zetu hasa wakatoliki na hata wale ambao si wakatoliki kwamba lazima  tulinde mazingira. Hii ni kama ishara ya vitendo lakini anawahimiza wengine pia wafanye hivyo na watunze mazingira kwa njia moja au nyingine

Mnaushirikiano upi na Shirika la Umoja wa Mataifa la  kulinda Mazingira ?

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP  lililopo hapa Nairobi tunaambiwa kwamba ni shirika la kipekee lililoko hapa Afrika na kwa hivyo tunashirikiana kwa karibu sana kwa sababu Umoja wa Maitafa una kitengo kinachoitwa Faith and Earth- yaani imani na mazingira hivyo basi sisi tunashirikiana nawao kwa vile wanajua kwamba wale watu ambao wanaeneza Imani wana watu wengi pia ambao wakionyeshwa  mifano na kusaidiwa wanaweza chukua hatua  kwa kulinda mazingira ya Climate Action and Climate Justice

Kwa maoni yako unafiriki Dini inastahili kuchukua nafasi gani katika kulinda mazingira?

Katika Bibilia  na pia  katika Koran tukufu tunajua kwamba mwanzoni mungu aliumba mazingira hivyo basi akatuweke kama wakristo vile ambavyo wakristo wanaamini kwamba alituweka katika lile shamba la Eden,hivyo basi sisi watu wa imani tunaambiwa kwamba lazima tuwe watu ambao wanatunza vyema mazingira kwa vile mwishoni tutatoa hesabu kwa mungu jinsi tulivyo fanya jukumu letu la kulinda mazingira hivyo basi ni Imani yetu na pia sio tu kwa sababu ya Imani. Mtakatifu Francisco amabye sisi tunamfuata kama kapuchini wa Francisco aliishi miaka 800 iliyopita kule Asizi Italia na kule tunaambiwa kwamba alianza kumshukuru mungu na ndipo sasa hata hilo jina la Udatusi Praise God  likaja ama tumshangilie mungu kwa sababu ametupa mazingira

 

Audio Credit
Jason Nyakundi
Audio Duration
2'50"
Photo Credit
World Bank/Curt Carnemark