Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafunzo ya FAO sasa yamewezesha hata waume zetu kufurahia kilimo- Paskazia

Mafunzo ya FAO sasa yamewezesha hata waume zetu kufurahia kilimo- Paskazia

Pakua

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea kubadilisha maisha ya wananchi kupitia miradi mbalimbali inayotekeleza huko nchini Tanzania.

Miradi hiyo ni pamoja na ule wa kupatia wakulima mbinu bora za kilimo ili kuongeza kipato, kulinda mazingira, kuepusha ukosefu wa chakula na  kutokomeza umaskini, mradi ambao unatekelezwa na FAO ambalo ni shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, kupitia mradi wa pamoja wa wa Umoja wa Mataifa kwa Kigoma. 

Miongoni mwa wanufaika wa miradi hiyo ni kikundi cha Umoja ni Nguvu, cha wanawake wa kata ya Katanga, wilaya ya Kakonko mkoaoi Kigoma ambako wameanza kushuhudia mafanikio na sasa wanafurahia. Assumpta Massoi akiwa mkoani Kigoma, alipata fursa ya kuwatembelea na kuzungumza nao na fuatana nao kwenye makala hii.

Audio Credit
Loise Wairimu/ Assumpta Massoi
Audio Duration
4'22"
Photo Credit
FAO Tanzania