Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hata sheria inatambua kuwa jukumu la malezi linapaswa kuwa la baba na mama

Hata sheria inatambua kuwa jukumu la malezi linapaswa kuwa la baba na mama

Pakua

Lengo namba 5 la Malengo ya maendeleo endelevu SDGs, inahimiza usawa wa kijinsia ili kuwafanya wanaume na wanawake katika jamii kuwa na usawa kwa mstakabali wa jamii nzima. Lakini lengo hilo limekuwa likipata misukosuko kutokana na mizizi ya kukosekana kwa usawa ambayo imekuwepo kwa miaka mingi na bado inatengenezewa mazingira ya kustawi pindi ambapo mtoto wa kike anawekewa mazingira ya kuendelea kubaki duni kutokana na kukosa fursa za elimu, mimba zisizotarajiwa na hata ndoa za utotoni.  Mazingira yote hayo, kwa mujibu wa Mwanasheria Cristina Manyama kwa kiasi fulani yanachangiwa na migogoro katika jamii hususani ndoa ambapo mama anaachiwa jukumu la kumlea mtoto wa kike. Adelina Ukugani wa redio washirika Storm FM ya Geita amemhoji Afisa huyu wa sheria anayetoa msaada wa kisheria kwa watu wasio na kipato nchini Tanzania, na hii ni makala yake.
 

 

Audio Credit
Adelina Ukugani
Audio Duration
3'44"
Photo Credit
UN Women/Ruth McDowall