Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

08 Mei 2020

08 Mei 2020

Pakua

  Leo katika Jarida la Umoja wa Mataifa  ikiwa ni Ijumaa ya mada kwa kina tunaangazia harakati za Ombeni Sanga, mvumbuzikijana mtanzania ambaye ametengeneza kifaa chenye uwezo wa kusambaza elimu katika mazingira ambayo hakuna mwalimu.

-Katibu Mkuu Antonio Guterres ametoa ombi lake la kimataifa kushughulikia na kupambana na kauli za chuki wakati huu wa COVID-19.

-Mafuriko makubwa, mizozo, nzige wa jangwani, uchumi uliodhoofika na janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19, vinatishia usalama na ustawi wa wakimbizi wa ndani milioni 2.6 nchini Somalia.

-Na, mikakati ya kutaka watu kubaki majumbani ili kuzuia kuenea kwa virusi vya ugonjwa wa Corona au COVID-19 imewaweka wafanyakazi njia panda akiwa hafahamu achague afe njaa na familia yake au afe kwa virusi. 

-Kwenye Neno la wiki, Dkt. Mwanahija Ali Juma kutoka BAKIZA anafafanua maana ya neno "PAKACHA"  

Audio Credit
UN News/Flora Nducha
Audio Duration
9'58"
Photo Credit
OCHA/Yaye Nabo Sène