Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machifu watumiwa Niger kuhamasisha dhidi ya COVID-19

Machifu watumiwa Niger kuhamasisha dhidi ya COVID-19

Pakua

Kwenye kitongoji cha Banizoumbou katika mji mkuu wa Niger, Niamey, Chifu Yaye Modi Alzouma, anahamasisha wananchi juu ya virusi vya Corona, akisema kuwa hata machifu wamekiri kuwepo kwa gonjwa hilo.

Hatua hii ya Chifu Alzouma ni sehemu ya kampeni zinazoendeshwa kwa ushirikiano na UNICEF zikijumuisha viongozi wa jadi na wapiga debe mjini Niamey.

Kampeni inalenga kuhamasisha jamii ielewa COVID-19, na izingatie kanuni za kutochangamana, na kuheshimu amri ya dharura ya kutotembea hovyo.

Chifu Alzouma anasema kuwa,“Tangu kuingia kwa huu ugonjwa huu wa Corona, tumekuwa tukifanya kazi kuongeza uelewa. Tunatuma magari yenye vipaza sauti kwenye makazi ya watu. Niamey ni mji mkubwa, kwa hiyo hatuwezi kutembea mguu kwa mguu. Ni kwa kutumia magari yenye vifaa mahsusi tunaweza kuelimisha watu. Watu wanasikiliza machifu. Machifu ndio wanawaelezea jinsi ya kuchukua hatua. Watu bado wanajaribu kuelewa hali ilivyo. Wakati wa sherehe za ubatizo au harusi, hawakusanyiki kwa sababu ya huu ugonjwa.”

Matumizi ya vipaza sauti vilivyofungwa kwenye magari yanapigiwa chepuo na Harouna Bague ambaye ni mpiga debe. Yeye anasema kuwa, “Watu wengi hawana televisheni wala radio na si kila mtu anaweza kufuatilia taarifa kupitia vyombo hivyo vya habari. Iwapo watu 5 watatusikiliza, wataweza kusambaza ujumbe huo kwa watu wengine 100 na kadhalika.”

Audio Credit
Flora nducha/Loise Wairimu
Audio Duration
1'57"
Photo Credit
© UNICEF/UNI322644/Haro