Ninachangia mapambano dhidi ya COVID-19 kwa kutumia talanta yangu-Babu Owino

6 Mei 2020

Taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, iliyotolewa hivi karibuni  imeonesha kuwa zaidi ya watoto milioni 127 wa shule za awali, shule za msingi na sekondari Afrika Mashariki na Kusini, ambao walitakiwa kurejea shuleni wiki hii, wanasalia nyumbani kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19. Hali hiyo inamtaka kila mtu kushiriki kwa namna yake kuhakikisha wanafunzi hawa wanaendelea kupata elimu wawapo nyumbani, hadi pale shule zitakapofunguliwa. Bob Owino, ni mbunge nchini Kenya ambaye ameamua kuitumia talanta yake ya masomo ya sayansi, kuwafundisha wanafunzi kupitia mitandao yake ya kijamii. Jason Nyakundi ameandaa makala kuhusu mbunge huyo.

Audio Credit:
Loise Wairimu/Jason Nyakundi
Audio Duration:
3'27"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud