Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chama cha wakunga Tanzania tunawashauri wakunga wote kutumia vifaa vilivyotakaswa wakati huu wa COVID-19:Lucy Mabada

Chama cha wakunga Tanzania tunawashauri wakunga wote kutumia vifaa vilivyotakaswa wakati huu wa COVID-19:Lucy Mabada

Pakua

 Dunia ikielekea kuadhimisha siku ya wakunga hapo kesho tarehe 5 Mei, Chama cha wakunga Tanzania (TAMA) kimewapa ushauri wakunga wote kuzingatia kuvaa vifaa muhimu vilivyotakaswa hususani wakati huu wa COVID-19 ili kuwalinda watoto dhidi ya maambukizi. Mwaka huu wa 2020 umetangazwa na Umoja wa Mataifa kuwa mwaka wa wa wauguzi na wakunga ili kutambua mchango mkubwa wa wahudumu hawa wa sekta ya afya. Warren Bright, Afisa Mkuu wa mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA Tanzania amefanya mahojiano na Lucy Mabada ambaye ni Mratibu kutoka Chama cha wakunga Tanzania.

 
 
 
 
 
 
 
Attachments area
 
 
 
Audio Credit
Loise/Warren Bright
Audio Duration
3'30"
Photo Credit
UNFPA