Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaendelea kukimbizana na muda kuzuia kusambaa kwa COVID-19 Sudan Kusini

UNHCR yaendelea kukimbizana na muda kuzuia kusambaa kwa COVID-19 Sudan Kusini

Pakua

 Katika eneo la Ajoung Thok, maafisa wa UNHCR wanafanya kazi kwa ukaribu na mashirika menmgine ya msaada wa kibinadamu pamoja na serikali ya Sudan Kusini kutoa elimu, kutibu na kuzuia uwezekano wa ugonjwa kusambaa. Watu wanaonekana wamesimama katika mistari ambaypo inawaonesha umbali unaotakiwa kati ya mt una mtu.

Takribani  watu milioni 1.6 wametawanywa ndani ya nchi na wengine 300,000 ni wakimbizi katika nchi yao. Wengi wanaishi katika hali ya msongamano bila maji, hali ya kujisafi na pia bila huduma ya afya. Wako katika hatari ya kuambukizwa virusi vya corona.

Mustafa Kur Lueth Kaman, ni afisa wa UNHCR anasema,

“Nilijua kuwa ni vigumu kwa mazoea haya kutekelezeka kwa dhati kwa kuzingatia muda: hata hivyo, tusipofanya, itawaweka watu hatarini. Ndiyo maana inatubidi kuichukua changamoto hii kwasababu tuko hapa mstari wa mbele kuhakikisha usalama wa wakimbizi unahakikishwa na pia wanapokea stahiki zao kwa heshima.”

Video zilizopigwa ardhini na hata kutokea juu kwa kutumia ndege isiyo na rubani, zinaonesha hali ilivyo iwe ni Bentiu, Juba na hata Ajoung Thok. Kambi zote zina msongamano, na zimesheheni watu wa rika zote, wazee kwa watoto. Mustafa Kur Lueth Kaman, Afisa wa UNHCR anaongeza,

"Lakini kwa kweli, bado tunaamini kuwa kuna idadi kubwa ya watu katika jamii ambao bado hawajauchukua ujumbe unaotolewa na ndiyo sababu tunahitaji kuendelea kuhamasisha hatua za kiafya na usalama zinaimarishwa au kutekelezwa na wakimbizi wenyewe. "

Ufadhili zaidi unahitajika kwa haraka kulinda na kuokoa maisha. UNHCR na wadau wanatoa sabuni na vifaa vingine vya kujisafi, kuongeza mgao wa chakula na wanaongeza uelewa ili kuwafikia watu wengi zaidi iwezekanavyo nchini kote.

Sauti
2'15"
Photo Credit
© UNHCR/Natalia Micevic