Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya changamoto za COVID-19 chanjo inaendelea Kenya:WHO

Licha ya changamoto za COVID-19 chanjo inaendelea Kenya:WHO

Pakua

Serikali ya Kenya kwa kushirikiana na shirika la afya duniani WHO wamesema licha ya changamoto kubwa iliyosababishwa na mlipuko wa janga la Corona au COVUD-19 wanajitahidi kuhakikisha watoto wanapata chanjo muhimu za kuokoa maisha.

Wamesema tayari mikakati ya kuhakikisha chanjo inawafikia wale wanaoihitaji zaidi imeanza kutekelezwa na wahudumu wa afya wanafanya kila wawezalo kuhakikisha COVID-19 haiwi kikwazo cha watoto kukosa chanjo muhimu kama za surua, polio, na magonjwa mengine hatari kwa afya ya mamilioni ya watoto. Kupata kwa kina kuhusu mikakati hiyo na chanjo inavyoendeshwa ungana na mwandishi wetu wa Nairobi Jason Nyakundi katika makala hii.

Audio Duration
4'32"
Photo Credit
PAHO.WHO.Jane Dempster