Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

28 APRILI 2020

28 APRILI 2020

Pakua

Katika jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

-Shirika la kazi duniani ILO leo likiadhimisha siku ya kimataifa ya usalama na afya kazini limetaka waajiri kuwalinda wafanyakazi wakati na baada ya janga la virusi vya corona au COVID-19

- Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC waliopona ugonjwa wa Corona waiasa jamii kuzingatia wito na masharti ya afya ili kujikinga na gonjwa hilo hatari

- Huko Cameroon kwenye kambi ya wakimbizi ya Gado mafunzo yanayotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi kwa hisni ya ufadhili wa Bill na Melinda Gates ya kulea watoto njiti kupitia mfumo wa kangaroo yaokoa maisha ya mamia ya watoto

-Makala yetu leo iko Kenya ikijikita na chanjo licha ya changamoto za janga la COVID-19

-Na mashinani utamsikia mtoto wa miaka 13 aliyepona ugonjwa wa Corona akieleza changamoto za ugonjwa huo

Audio Credit
UN News/Flora Nducha
Sauti
12'12"