Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanafunzi Tanzania kujifunza kupitia redio na televisheni kutokana na COVID-19

Wanafunzi Tanzania kujifunza kupitia redio na televisheni kutokana na COVID-19

Pakua

Wanafunzi Tanzania kujifunza kupitia redio na televisheni kutokana na COVID-19

Nchini Tanzania, wito wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, wa kuhakikisha wanafunzi wanaendelea kujifunza hata wakati wa huu wa kusalia majumbani kutokana na janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19, umeanza kutekelezwa ambapo hii leo Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imezindua rasmi urushaji wa vipindi vya masomo kupitia televisheni na Radio.

Uzinduzi huo umefanywa kwenye mji mkuu wa Tanzania Dodoma na Katibu Mkuu wa  Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo ambapo amesema.

(Sauti ya Dkt. Leonard Akwilapo)

Vipindi hivi ni vya masomo mbalimbali kwa ngazi ya elimu ya awali,elimu ya msingi na elimu ya kutoka Kidato cha  cha kwanza mpaka cha sita,vipindi hivi vitasambazwa katika vyombo mbalimbali vya habari huku nchini ili masomo yaweze kufikia wanafunzi wetu nchi nzima

Lengo kubwa la kutoa vipindi hivi ni kuwaezesha wanafunzi waendelee kujifunza wakati huu ambapo wako nyumbani,katika kipindi hiki ambapo shule zao zimefungwa.

 

Dkt.Akwilapo amesema wizara yake iliandaa vipindi hivyo kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania. Lakini vipi kuhusu lugha?

 

 

(Sauti ya Dkt. Leonard Akwilapo)

Hata hivyo urushwaji wa vipindi hivi hauna maana ya kuwa mbadala wa masomo ya darasani mara baada ya shule hizi kufunguliwa baada ya janga hili kuwa limekwisha. Kwa hivyo tunawasihi walimu wataendelea na mitaala yao kama inavyoelekezwa kwenye taratibu zetu za kila siku sio kwamba wataruka mambo ambayo yatakuwa yamerushwa kwenye vipindi hivi.

Akaenda mbali zaidi kuzungumzia wanafunzi wa kidato cha sita waliokuwa wafanya mitihani.

(Sauti ya Dkt. Leonard Akwilapo)

Maandalizi ya vipindi hivi yamezingatia lugha ambazo ni za kufundishia ambazo ni Kiswahili na Kingereza kwa ngazi ya elimu ya msingi kwa sababu tuna shule ambazo ni za serikali ambazo zinafundishia kwa kiswahili na zile za binafsi ambazo zinafundishia kwa kingereza .Lakini kwa upade wa shule za sekondari  kama kawaida ni lugha ya kingereza

 

Baraza la mitihani la Tanzania limeandaa vipindi  kwa ajili ya maandalizi ya watahiniwa wa kidato cha sita nayo pia yatarushwa kwenye vyombo hivi.

Vipindi hivi vitawawezesha watahiniwa hawa kufanya marudio ya mada mbalimbali amdazo wataalam wa baraza la mitihani wameona ni vizuri zikafanyiwe marejeo  nadhani walikuwa wanaangalia mada ambazo zinakuwa na maswali magumu wakati wa kufanya mtihani.

 

 

 

Katibu Mkuu huyo amesema vipindi hivyo havitakuwa mbadala pindi shule zitakapofunguliwa na kwamba walimu wataendelea kufundisha kwa kufuata mitaala hata kama kuna matangazo ya radio na televisheni.

 

 

Audio Credit
UN News/Flora Nducha
Audio Duration
2'40"
Photo Credit
UNICEF/Tapash Paul