Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mvua za kiholela zinatuchanganya- wakulima

Mvua za kiholela zinatuchanganya- wakulima

Pakua

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, ni mabadiliko ya tabianchi. Suala hili limezua sintofahamu miongoni mwa wakazi wa dunia hii kutokana na mabadiliko ya misimu ya mvua, jua na hata kupata vipindi vya mvua kupita kiasi. Wakulima wamechanganyikiwa bila kufahamu la kufanya. Miongoni mwao ni wakulima kutoka Boza wilaya ya Pangani mkoani Tanga nchini Tanzania. Uelewa wake kuhusu mabadiliko ya tabianchi uko vipi? Ungana basi na Saa Zumo wa radio washirika Pangani FM kutoka Tanzania.

Audio Credit
Loise Wairimu/Saa Zumo
Audio Duration
3'51"
Photo Credit
World Bank/Curt Carnemark