Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jumuiya ya wanakiswahili ulimwenguni na duniani kote imehuzunika sana

Jumuiya ya wanakiswahili ulimwenguni na duniani kote imehuzunika sana

Pakua

Miongoni mwao ni Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili huko Zanzibar BAKIZA. "Profesa Ken Walibora ni Mtaalamu ni Mwandishi wa habari ni mwandishi wa vitabu ni Mwalimu lakini ni  mwanafastafa muhimu katika taaluma ya lugha ya kiswahili.Alikua tayari kuwakosoa baadhi ya watu kwa kuandika makala mbalimbali kwa kupitia magazeti na hasa gazeti la Taifa leo linalotoka kule  Kenya. Lakini pia alikua tayari kuandika kazi za fasihi katika njia tofauti. Kitabu chake kimoja chake ambacho ni msana ni  Siku Njema A good day  kimetafsiriwa kwa lugha ya kingereza na kifaransa ni riwaya nzuri ambayo inaelezea  mambo mengi na muhimu ya kimaisha .Jumuia ya wanakiswahili ulimwenguni na duniani kote imehuzunika sana."

Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi wa Baraza la Kiswahili Tanzania, BAKITA naye akafunguka, "Kikubwa zaidi ambacho Profesa Ken Walibora tunaweza tukamkumbuka ni pale ambapo alijaribu  kwa kushirikiana na wenzewe kuandika Islahi mbalimbali katika programu ya Microsoft na Google za kiswahili. Mwafrika wa mashariki mwenzetu  ambaye alidhubutu na kujaribu kuingiza hizo isilahi za komputer katika mzuguko wa matumizi yake ya kawaida

Kwa hivyo Kifo cha Ken Walibora sio tu  kwamba kimeigusa familia mbali pia  kimewajusa familia ya waswahili wote waliofundishwa naye,Vyoo amabayo amehudhuria  hata Marekani,Nchi mbalimbali,Kenya alikofanya kazi kama mwanahabari lakini pia amefanya kazi kubwa  ya kuandika vitabu ambavyo ameacha kama kumbukumbu katika uga huu wa lugha . Hivyo ni vitu ambavyo sitaweza kumsahau Profesa Ken Walibora."

Leonard Mambo Mbotela, mtangazaji nguli wa siku nyingi nchini Kenya, alikuwa rafiki wa karibu na mwendazake Ken ambapo akihojiwa na mwandishi wetu wa Nairobi, Kenya, Jason Nyakundi, kuhusu kifo cha Ken, anasema,,

(Sauti ya Leonard Mambo Mbotela)

Na vipi kuhusu kitabu ambacho Profesa Ken alikuwa anaandaa kuhusu Mambo Mbotela?

(Sauti ya Leonard Mambo Mbotela)

"Alikuja kwangu ananiambia  Bwana Mambo wewe ni mtangazaji mashuhuri mwanahabari mashuhuri  waonaje kama tukija na kitabu kuhusu maisha yako?Nikamwambie Ken, hilo ni wazo nzuri sana niko tayari  endelea.Nilipomjibu naama hiyo tukapanga basi akaja hapa nyumbani kwangu Langata akanihoji na kupiga picha na kadhalika .Akaniambia  sasa anaenda kuandika hicho kitabu Kabla hajafa akanipigia simu na akaniambia naja  nyumbani turekebishe mawili matatu na kweli akaja hapa nyumbani tukakaa wiki tatu zilizopita tu  tukaskizana na  akatoka akashika njia akaenda. Akaniambia usijali ntakupigia  tutapangapanga Mwezi wa May Mungu akipenda tutalaunch kitabu. Hivyo ndivyo nilivyo kuwa na mpaka leo hii Kitabu hizo alikiachia msaidizi wake ambaye amenipigia simu leo leo tu  akiniambia kwamba Ken ametuwacha lakini Kitabu kitaendelea na tutafanya lauch mwezi huu wa tano."

Audio Credit
Arnold Kayanda/ Mwanahija Ali Juma/ Onni Sigalla/ Mambo Mbotela
Audio Duration
4'39"
Photo Credit
IOM/A. Deng 2018