Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kazi ya bodaboda imeboresha maisha yangu na mume wangu-Cecilia Paul

Kazi ya bodaboda imeboresha maisha yangu na mume wangu-Cecilia Paul

Pakua

Pamoja dunia hivi sasa kuwa na changamoto mpya kama mlipuko wa ugonjwa COVID-19, lakini mipango ya muda mrefu inaendelea kutekelezwa ili kutimiza kusudio kuu la kuyatimiza kwa ukamilifu malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs ifikapo mwaka 2030. Malengo yote kwa ujumla wake yanakusudia kuifanya dunia kuwa mahali bora pa kuishi na ili kufikia hapo ni jukumu la kila mtu kushiriki harakati hizi. Cecilia Paul ni mwanamke ambaye kupitia kazi ya kuendesha pikipiki anachangia, miongoni mwa malengo mengine, lengo namba moja la kutokomeza umaskini na lile la la tano la usawa wa kijinsia kwani anaweza kujipatia hadi shilingi elfu 15 fedha ya Tanzania sawa na takribani dola 7 za Kimarekani. Makala hii iliyoandaliwa na Nyota Simba inasimuliwa na Evarist Mapesa kutoka redio washirika SAUT FM.

Audio Credit
Loise Wairimu/ Evarist Mapesa
Audio Duration
3'45"
Photo Credit
Benki ya Dunia/Stephan Gladieu