16 APRILI 2020
Miongoni wa habari ambazo Flora Nducha anakuletea katika Jarida la Umoja wa Mataifa hii leo
- Ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni na hali ya kutovumiliana vimeongezeka wakati huu wa mlipuko wa virusi vya Corona au COVID-19 kwa mujibu wa mtaalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Tendayi Achiume
-Huko Congo DRC visa vipya vya Ebola vimeripotiwa huku taifa hilo la maziwa makuu likiendelea kukabiliana na majanga mengine kama COVID-19,utapiamlo na vita limesema shirika la afya duniani WHO.
-Nchini Kenya mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wa imarisha afya ya mama na mtoto waleta nuru kwa maisha ya maelfu ya watu
-Makala yetu inatupeleka Tanzania kukutana na mwanamke mjasiriamali na mpambanaji anayeendesha bodaboda kukidhi mahitaji ya familia yake
-Na mashinani tunabisha hodi Kenya kwa mwalimu anayetumia mbinu bunifu kuhakikisha wanafunzi wake wanasoma wakati huu wa COVID-19