Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres ametoa wito kwa ulimwengu mzima kujifunza kwa nchi ya Rwanda na watu wake

Guterres ametoa wito kwa ulimwengu mzima kujifunza kwa nchi ya Rwanda na watu wake

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa ulimwengu mzima kujifunza kwa nchi ya Rwanda na watu wake kwa namna walivyomudu kuponya majeraha ya athari mbaya za maujai ya kimbari dhidi ya watutsi , Grace Kaneiya na maelezo zaidi

(Taarifa ya Grace Kaneiya )

Ikiwa leo dunia inaadhimisha kumbukumbu ya mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi nchini Rwanda ambapo watu zaidi ya milioni moja waliuawa ndani ya siku 100, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameanza kwa kusema kuwa siku hii inawaenzi wale wote waliouawa, wengi wakiwa watutsi pamoja na wahutu na watu wengine ambao waliyapinga mauaji ya kimbari. Bwana Guterres amesema,

(Sauti ya Guterres)

 "na tunapata msukumo kutoka kwenye uwezo wa wale ambao walinusurika kwa kuwa na maridhiano na urejeaji katika maisha ya kawaida. Hatupaswi kamwe kuruhusu ukatili kama huo kutokea tena.”

Aidha Bwana Guterres amesema kuwa wanadamu wanapaswa  kusema hapana dhidi ya kauli za chuki na ubaguzi, na kukataa kujitenga, utaifa na uwekaji wa mipaka.

Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kwa kutambua tu kwamba sisi sote ni familia moja ya wanadamu ndani ya sayari moja ndipo tutaweza kuzimudu changamoto nyingi za ulimwengu ambazo zinatukabili - kutoka kwa COVID-19 hadi mabadiliko ya tabianchi na kisha akasema,

(Sauti ya Guterres)

 “tangu mauaji ya kimbari, Rwanda imeonesha kuwa inawezekana kunyanyuka kutoka katika majivu, kupona na kujenga upya jamii imara na iliyoendelevu zaidi. Tunapoangalia mbele kuongeza kasi ya juhudi za kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, wacha tuchukue funzo kutoka katika somo linaloendelea la Rwanda.”

Audio Credit
Assumpta Massoi/ Grace Kaneiya
Audio Duration
1'43"
Photo Credit
UN/Milton Grant