Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukata kwenye WFP walazimisha kupunguza mgao Uganda

Ukata kwenye WFP walazimisha kupunguza mgao Uganda

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani (WFP) limekata msaada wake wa chakula na pesa kwa wakimbizi zaidi za milioni 1.2 nchini Uganda kutokana na ukata wa ufadhili wakati huu ambapo dunia imezongwa na changamoto ya kupambana na mlipuko wa virusi vya Corona, COVID-19. Haya hapa maelezo zaidi na mwandishi wetu John Kibego kutoka Uganda.
(Taarifa ya John Kibego.)
Shirka hilo limekata msaada wake wa chakula kwa asilimia 30 na pia kwa wale waliokuwa wakipokea pesa taslimu.
Afisa wa mawasilaino wa shirika la mpango wa chakula duniani (WFP) cnini Uganda Lydia Wamala ameiambia idhaa hii kwamba hatua hiyo imechukuliwa kutokana na pengo la ufadhili la dola milioni 137 za Kimerekani uliotarajiwa mnamo mwaka huu wa 2020.
Amesema hawajawa na chaguo na kuongeza kuwa kuna hatari ya kupunguza msaada huo zaidi kwa asilimia 15 ikiwa hawatapata ufadhili wa angalao dola milioni 96 za Kimarekani mnamo mwaka huu.
Hata hivyo Wamala amesema ukata huu hautaathiri wakimbizi wapya waliowasili katika kipinidi cha miezi mitatu iliopita na pia WFP itaendelea kujitahidi kutoa chakula sitahili kwa watoto wanaokabiliwa na utapiamlo, wajawazito na wanonyonyesha watoto kulingana na ufadhili uliopo.
WFP inaonya kwamba ukosefu wa mahitaji ya msingi kama chakula kwa wakimbizi unadidimiza matumaini na mustakbali wao ukiwaweza hatarini kwa matatizo mengine mengi zaidi.
Je, wakimbizi wamepokeaje hatua hii?
Nimezungumza na mkimbizi Edson Nzeimaana Jmahuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye sasa anaishi katikamakaazi ya wakimbizi ya Kyangwali.
(Sauti ya Edson Nzeimaana 1)
Na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa.
(Sauti ya Edson Nzeimaana 2)

 

Audio Credit
Assumpta Massoi/ John Kibego
Audio Duration
2'6"
Photo Credit
WFP