Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

3 Aprili 2020

3 Aprili 2020

Pakua

ASSUMPTA: Hujambo na karibu kusikiliza jarida kutoka Idhaa ya Kiswahili  ya Umoja wa Mataifa mimi ni ASSUMPTA MASSOI nikiwa hapa hapa New York Marekani

 

JINGLE (04”)      

 

ASSUMPTA: Ni Ijumaa  ya April  03 mwaka 2020 na kama ilivyo ada leo ni mada kwa kina ambapo leo tutamsikiliza mtaalamu wa afya upande wa tatizo la usonji akitueleza kinagaubaga kuhusu tatizo hilo.  Kwanza tupate Habari kwa Ufupi, ikiwasilishwa na Grace Kaneiya. 

====================================================

STUDIO: Play Habari kwa UFUPI

 

                                      HABARI KWA UFUPI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo amezungumza na waandishi wa habari kwa njia ya video kutathmini ombi lake alilotoa siku 10 zilizopita kutaka sitisho la chuki na mapigano duniani ili kuimarisha harakati dhidi ya janga la virusi vya Corona, au COVID-19.

Guterres amesema pande kinzani kadhaa zilitikia wito kama vile Sudan Kusini, Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Yemen.

 

(Sauti ya Antonio Guterres)

“Lakini kuna tofauti kubwa kati ya azimio na vitendo, kati ya kutekeleza amani kwa vitendo na katika maisha ya watu. Kuna ugumu kwenye utekelezaji kwa kuzingatia kuwa mzozo umedumu muda mrefu na kuna kutokuaminiana na kuna wachonganishi na shuku. Kwingineko mapignao yameshamiri. Tunahitaji juhudi thabiti za kidiplomasia kukabili changamoto hizi.”

=====================

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, bado lina hofu kubwa juu ya ongezeko la ghasia nchini Burkina Faso, ghasia ambazo kila uchao zinafurusha watu kutoka kwenye makazi yao. Sambamba na ghasia hizo ambazo zimekumba pia wakimbizi kutoka Mali ambao wameona bora warejee nyumbani, mlipuko wa virusi vya Corona, au COVID-19 nao pia umekuwa chumvi kwenye kidonda kwa wakimbizi hao ambao sasa ugenini ni kuchungu na nyumbani ni kuchungu.

 

==============

 

NA, Umoja wa Mataifa umesema pamoja na hatua kubwa zilizopatikana katika kukabiliana na mabomu ya kutegwa ardhini kote duniani , mabomu hayo bado ni tishio kubwa . Hayo yamo katika ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wa kuelekea maadhimisho ya siku ya kimataifa ya uelimishaji umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini itakayokuwa kesho Jumamosi.

 

 

MWISHO WA HABARI KWA UFUPI

 

ASSUMPTA : Asante sana Grace Kaneiya kwa mukhtasari huo wa habari. 

 

STUDIO: Play Midwaysting

 

ASSUMPTA: Naam, na sasa ni wasaa wa mada yetu ya leo tukiangazia usonji. Godfrey Kimathi ni mtaalamu mbobevu wa tatizo hilo (nitatafuta anatambulishwa) ambaye pia ni rais wa wataalam wa usonji nchini Tanzania anaanza kwa kueleza usonji ni nini na dalili zake ni zipi?

USONJI CLIP 1

Shukrani Dkt Kimathi, lakini tatizo la usonji husababishwa na nini?

USONJI CLIP 2

Na je, usonji unatibika?

USONJI CLIP 3

====================================================

STUDIO: PLAY- 2. MADA KWA KINA

 

ASSUMPTA: Shukrani sana Dkt Godfrey Kimathi kwa makala hii. Na sasa ni wakati wa kujifunza Kiswahili , Je wafahamu tofauti za maneno "MRUNDIKANO NA MLUNDIKANO”? basi ungana na mchambuzi wetu Onni Sigalla Mhadhiri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili  la Taifa Tanzania , BAKITA kwa ufafanuzi

 

STUDIO PLAY NENO LA WIKI

 

 

STUDIO PLAY BRIDGE for 5 Second then hold under

 

====================================================

ASSUMPTA : Shukrani sana Onni Sigalla  kwa ufafanuzi huo.

====================================================

STUDIO: BRING UP BRIDGE for 5 Second then hold under

 

====================================================

ASSUMPTA: Na kufikia hapo ndivyo nahitimisha jarida letu kwa leo. Basi hadi wakati mwingine kwa habari na makala kutoka Idhaa ya Kiswahili ya  Umoja wa Mataifa.  Unaweza kupata matangazo na taarifa nyingine na kujifunza Kiswahili kwenye wavuti wetu news.un.org/sw. Kwa niaba ya msimamizi FLORA NDUCHA na wote walioshiriki kufanikisha Jarida hili, kutoka hapa Marekani mimi ni ASSUMPTA MASSOI, ninakutakia mwisho mwema wa wiki na  Kwaheri. 

 

TAPE: CLOSING BAND

===================

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
9'58"