Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya yatangaza visa vipya vya COVID-19 na kufikisha idadi ya wagonjwa hadi 81

Kenya yatangaza visa vipya vya COVID-19 na kufikisha idadi ya wagonjwa hadi 81

Pakua

Wagojwa wawili ambao wamethibitishwa kupona virusi vya corona nchini Kenya wameonekaa hadharani kwa mara ya kwanza leo wakati wakizungumza kwa njia ya video na Rais Uhuru Kenyatta na kuonyeshwa kwenye runinga kadhaa nchini Kenya. Hata hivyo wizara ya afya nchini Kenya imatangaza uwepo kwa wagonjwa 22 zaidi wa virusi vya corana hii leo na kufanya idadi jumla kufikia wagonjwa 81. Jason Nyakundi anayo taarifa kamili

(TAARIFA YA JASON NYAKUNDI)

Hii ndiyo mara ya kwanza waathiriwa hao wa virusi vya corona kwa majina Brenda na Brian na ambao sasa wamepona wameonekana hadharani.
Brian na Brenda walifanya mazungumzo na rais Kenyatta ambapo Rais aliwashauri wakenya kusaidia katika kuzuia maambukizi ya virusi hivyo hatari.
Brenda ndiye mgonjwa kwanza na Brian mgonjwa wa tatu kupona kutokana na virusi vya Corona nchini Kenya.
Akitangaza hilo waziri wa afya Mutahi Kagwe amewataka wakenya kufuata kanuni zinaohitajika ili kusaidia kupigana na virusi hivyo hatari vya corona.
(SAUTI YA KAGWE 1)
 
Awali waziri Kagwe pia alisema kuwa maambukizi mapya yanatokana na usafiri wa bodaboda, ambao upo katika kila kona ya nchi, ambapo alitoa kanuni mpya kwa waendeshaji wa bodaboda ili kuzuia maambukizi kati yao na wateja wao.
 
Alisema kuwa kwa watakaokaidi kanuni hiyo watalazimishwa na maafisa wa polisi.
 
(SAUTI YA KAGWE 2)
 
 Hadi leo Jumatano wagonjwa waliothibitishwa kuwa na virusi vya corona nchini Kenya wamefikia watu 81 kwa mujibu wa wizara ya afya baada ya wagonjwa 22 kuthibitishwa leo.
 
Wizara ya afya inasema kuwa wagonjwa 21 kati 22 waliogunduliwa kuwa na virusi vya corona tayari walikuwa katika karantini.
 
Katika upande mwingine wizara hiyo ya afya imeonya kuwa huenda maambukizi yakawa makubwa zaidi kuanzia wiki ya kwanza ya mwezi Aprili.
 
Mkurugenzi katika wizara ya afya Dr Patrick Amoth amesema huenda hata hadi watu 10,000 wakaambukizwa virusi vya Corona nchini Kenya ifikapo mwisho mwa mwezi Aprili.
 
(SAUTI YA AMOTH)

Audio Credit
Assumpta Massoi/ Jason Nyakundi
Audio Duration
3'31"
Photo Credit
UN Kenya/Newton Kanhema