26 MACHI 2020
Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea
-Visiwa vya Zanzibar nchini Tanzania vyachukua hatua kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona COVID-19 ikiwemo kupunguza mrundikano magerezani
- Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema COVID-19 isiwe chanzo cha kusahau huduma muhimu za chanjo kwa watoto
-Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limewachagiza wahamiaji kuingia katika sekta ya kilimo likisema jembe halimtupi mkulima
-Makala yetu leo inatupeleka nchini Tanzania ambapo tutasikia kutoka kwa afisa habari wa wizara ya afya nchini humo kuhusu mapambano dhidi ya virusi vya corona.
-Na mashinani utamsikia Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet akizungumzia virusi vya Corona na wafungwa magerezani