24 Machi 2020

24 Machi 2020

Assumpta Massoi : Hujambo na Karibu kusikiliza Jarida kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, kutoka hapa New York Marekani.

JINGLE (04”)      

ASSUMPTA:Ni jumanne  ya  Machi Ishirini na nne mwaka 2020, mwenyeji wako studioni hii leo ni mimi ASSUMPTA MASSOI 

1: Tunapopambana na COVID-19 tusiyape kisogo maradhi kama TB:WHO 
Tunapopambana na janga la kimataifa la afya COVID-19 ni wakati pia wa kutafakari na kutoyapa kisogo maradhi mengine makubwa ikiwemo kifua kikuu au TB, amesema mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani WHO. Flora Nducha na taarifa zaidi

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Mkurugenzi huyo Dkt. Tedros Adhamon Ghebreyesus ameikumbusha dunia na kila mtu kwamba ingawa virusi vya corona, COVID-19 ndio vinavyogonjwa vichwa vya habari kila kona ya dunia kuna gonjwa lingine la mfumo wa hewa ambalo ni chagamoto kwa dunia

(SAUTI YA DKT. TEDROS CUT 1)
“Kuna ugonjwa mwingine wa mfumo wa hewa ambao unazuilika na kutibika lakini unakatili Maisha ya watu milioni 1.5 kila mwaka na gonjwa hilo la muda mrefu ni kifua kikuu.”

Ameongeza kuwa wakati dunia leo ikiadhimisha siku ya kifua kikuu duniani ambayo kila mwaka hua Machi 24, hii nifursa ya kuwakumbusha viongozi wa dunia kuhusu wajibu wao wa ahadi waliyoiweka ya kutokomeza madhila na vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huu mbaya na wa muda mrefu wa TB.

(SAUTI YA DKT. TEDROSS CUT 2)
“Dunia inachukua hatua muafaka na za haraka kukabiliana na COVID-19, tunatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kukumbatia lengo na uharaka huo kwa vita dhidi ya kifua kikuu na kwa kuwa na dunia yenye afya, salama na ya usawa kwa kila mtu.”

Kaulimbiu ya siku ya mwaka huu ni “wakati umewadia kutokomeza TB” na tawkimu za WHO zinaonyesha kwamba kifua kikuu au TB ni ugonjwa wa kuambukiza unaokatili Maisha ya watu wengi zaidi duniani.

Kila siku zaidi ya watu 4000 wanakufa kutokana na TB na wengine zaidi ya 30,000 wanaugua ugonjwa huu ambao unazuilika na kutibika.

Na katika kuhakikisha gonjwa hili linatokomezwa WHO imetangaza muongozo mpya kuhusu matibabi ya kifua kikuu ambao utasaidia kuwa na matokeo mazuri ya tiba kwa wagonjwa kuokoa maisha.

Tangu mwaka 2000 Who inasema juhudi za kimataifa za kukabiliana na kifua kikuu zimeokoa Maisha ya watu milioni 58.

===================================================

2: Uganda sasa ina wagonjwa wanane wa COVID-19 vyatibitishwa, Uganda

Nchini Uganda serikali imeimarisha juhudi za kudhibiti virusi vya Corona COVID-19 baada ya kuthibitishwa kwa wagonjwa wapya wanane katika nchi hiyo na kuwaacha wanchi wakiwa katika hali ya taharuki. Miongoni mwa hatua mpya zilizochukuliwa sasa ni uamuzi wa kufunga masoko ambayo yalikuwa yameaachwa  wazi sna kusababisha bei ya bidhaa muhimu kupanda. Maelzo zaidi katika taarifa ya John Kibego 
(Taarifa ya John Kibego)

====================================================
STUDIO. MIDWAYSTING
====================================================
ASSUMPTA: Punde ni makala na leo tunakwenda Kenya kusikiliza makala kuhusu Kifua Kikuu na hatari za usugu wa dawa, usibanduke.

====================================================

3: Ondoeni vikwao kusaidia COVID-19, madaktari wasemao ukweli msiwaadhibu- Bachelet
 
Wakati idadi ya wagonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 ulimwenguni ikizidi kupaa na kuwa zaidi ya 330,000 huku vifo vikifikia 1,4652, Kamishna Mkuu wa haki za binadamu, Michelle Bachelet ametaka vikwazo vya kisekta duniani viondolewe ili mataifa yaweza kukabiliana na mlipuko wa virusi hivyo. Grace Kaneiya na ripoti kamili.
 
(Taarifa ya Grace Kaneiya)
 
Taarifa iliyotolewa leo mjni Geneva, Uswisi na ofisi ya yake, imemnukuu Kamishna Mkuu Bachelet akisema kuwa vikwazo hususan katika sekta ya afya vinaweza kusababisha maambukizi na vifo zaidi na hata kusambaratisha mifumo ya afya.
 
“Misingi ya kibinadamu inapaswa kuzingatiwa kwenye vikwazo hivyo haraka hususan kwenye vifaa vya matibabu na dawa,”  amesema Bi. Bachelet akitolea mfano Iran ambako amesema watu wapatao 1,800 wameshafariki dunia kutokana na COVID-19 kwa sababu vikwazo vinakwamisha wao kupatiwa vifaa kama vile vivutia hewa na vifaa vya  kusaidia wahudumu wa afya kujikinga dhidi ya virusi.
 
Bi. Bachelet amesema zaidi ya madaktari 50 wamefariki dunia nchini Iran tangu wagonjwa wa awali wathibitishwe nchini humo wiki 5 zilizopita, “janga la Corona linasambaa nchi jirani na litakuwa na madhara kwenye mifumo ya afya kwa nchi za Pakistani na Afghanistan.”
 
Amegusia kuwa vikwazo vya aina mbalimbali vinaweza pia kukwamisha huduma za kitabibu dhidi ya Corona huko Cuba, Korea Kaskazini, Venezuela na Zimbabwe ambako amesema baadhi yao tayari mifumo ya afya ni dhaifu.
  
Amekumbusha kuwa ni muhimu kulinda afya za watoa huduma na kwamba madaktari hawapaswi kuadhibiwa kwa kubainisha udhaifu wanaokumbana nao wanapokabiliana na janga la Corona kwa kwa wao wako mstari wa mbele kumlinda kila mtu,
 
Bi. Bachelet ametoa wito kwa viongozi duniani kuwa kitu kimoja akisema mshikamano wa kimaitafa ni muhimu wakati wote katika kusongesha haki za binadamu na kwamba ni muhimu katika kusongesha maslahi ya kila taifa katika kipindi cha sasa.
 
COVID-19 imethibitishwa katika mataifa 189.

===================================================
STUDIO: Play MUSIC 4 for 5 seconds and hold under
====================================================
ASSUMPTA:  Na sasa ni makala ambapo mwandishi wetu wa Nairobi, Kenya ameandaa makala kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu, au TB ikiwa leo ni siku ya TB duniani na amezungumza na  Dkt. Jeremiah Jakaya ambaye anaanza kwa kuelezea hatari anayopata mgonjwa wa TB anapougua virusi vya Corona au Covid-19.
=================================================
STUDIO: PLAY MAKALA
==================================================== 

ASSUMPTA: Play MUSIC 4 for 5 seconds and hold under
====================================================
ASSUMPTA:  

Shukrani sana Jason Nyakundi na wote mlioshiriki kwenye makala hiyo.

====================================================
Na sasa ni  mashinani tuungane naye  Abdalla Majura mmoja wa wafanyakazi wenye ulemavu katika hospitali ya  CCBRT jijini Daresalaam nchini Tanzania akitoa ushauri kwa serikali kutia mkazo kwenye mabasi ya abira ya umma, maarufu kama daladala ili kuzuia maambukizaji ya virusi vya Corona.
====================================================
Studio: Play Mashinani
====================================================
ASSUMPTA: 
Asante sana Abdalla Majura kwa ujumbe huo.
==================================================
STUDIO: Play Bridge
ASSUMPTA: Na hadi hapo natamatisha jarida letu la leo. Hadi wakati mwingine kwa habari na makala kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa unaweza kupata matangazo na taarifa nyingine na kujifunza Kiswahili kwenye wavuti wetu news.un.org/sw. Msimamizi  wa matangazo ni FLORA NDUCHA na fundi mitambo na mimi ASSUMPTA MASSOI, nasema kwaheri kutoka New York. 

==================================================
TAPE: CLOSING BAND

Audio Credit:
Assumpta Massoi
Audio Duration:
12'51"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud