TB ikichanganyika na COVID-19 ni janga juu ya janga

24 Machi 2020

Ugonjwa wa Kifua Kikuu au TB, bado umesalia kuwa miongoni mwa magonjwa hatari zaidi duniani. Zaidi ya watu 4000 hupoteza maisha yao  kila siku kutokana na ugonjwa TB huku 30,000 wakiwa wanapata maambukizi ya ugonjwa huu unaoweza kuzuiwa na kutibiwa. Gonjwa hili linasalia kuwa tishio wakati huu ambapo kumeibuka virusi vya ugonjwa wa Corona au COVID-19 ambao nao umetikisa dunia ukisambaa katika mataifa 189 na ukiwa umesababisha vifo vya watu zaidi ya 14,500 tangu kubainika mwezi Desemba mwaka jana. Ugonjwa huu nao unaathiri mapafu na ni kwa mantiki hiyo katika maadhimisho ya siku ya kutokomeza TB duniani hii leo tunaangazia hatari ya COVID-19 kwa mtu aliyeugua TB na mwandishi wetu wa Nairobi, Kenya amezungumza na Daktari Jeremiah Jakaya kufahamu hilo naye hakusita kwa kuanza kuchambua katika makala hii

Audio Credit:
Jason Nyakundi
Audio Duration:
4'

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud