Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

18 Machi 2020

18 Machi 2020

Pakua

Assumpta Massoi : Hujambo na Karibu kusikiliza Jarida kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, kutoka hapa New York Marekani.

JINGLE (04”)      

ASSUMPTA:Ni Jumatano ya  Machi kumi na nane mwaka 2020, mwenyeji wako studioni hii leo ni mimi ASSUMPTA MASSOI 

1: COVID-19 Tanzania : Wagonjwa wafikia 3, Vyuo Vikuu vyafungwa, mgonjwa wa kwanza azungumza.
 Nchini Tanzania idadi ya wagonjwa wa Corona au COVID-19 imefikia 3 baada ya wagonjwa wapya wawili kuthibitishwa hii leo wakiwa ni raia wa Marekani na Ujerumani. Taarifa zaidi na Flora Nducha.
 (Taarifa ya Flora Nducha)
 Taarifa za kuthitbishwa kwa wagonjwa hao wapya zimetolewa leo mjini Arusha nchini Tanzania na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
 (Sauti ya Ummy Mwalimu)
 “Sampuli ya kwanza ni ya raia wa Marekani mwenye umri wa miaka. 61 ambaye ni mkazi wa Dar es salaam. Mgonjwa huyu sasa hiv iamewekwa mahala maalum kwa ajili ya taratibu nyingine za matibabu ikiwemo kufuatilia watu waliokuwa karibu naye.  Sampuli ya pili ambayo imefanyiwa vipimo na kuthitishwa kuwepo kwa virusi vya Corona ilipokelewa kutoka Zanzibar ambayo ilipokelewa kutoka Zanzibar ni ya mwanaume mwenye umri wa miaka 24 raia wa Ujerumani.”
 
Waziri Ummy akatoa wito kwa wananchi..
 
(Sauti ya Ummy Mwalimu)
 
“Kutokuwa na hofu kwa kuwa serikali inaendelea kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa ugonjwa huu unadhibitiwa nchini kwetu.”
 
Na hatua zaidi za kudhibiti kusambaa kwa COVID-19 zikatangazwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jijini Dar es salaam.
 
(Sauti ya Kassim Majaliwa)
Sasa leo tunaendelea kuongeza vyuo vya elimu ya kati na Vyuo Vikuu vyote nchini navyo pia tunasitisha kuendelea na masomo. Tunatambua Vyuo Vikuu wanafunzi wengi wako likizo na sasa tunawataka wasirudi kwenye vyuo vyao, na wale wachache waliokuwa wamebaki kwa mitihani nao pia waondoke mara moja  kwenye vyuo hivyo ili kuondoa  misongamano kwenye maeneo hayo. Bado shughuli za maduka na masoko zitaendelea. Na natamka hili kwa sababu tumeanza kuona mkanganyiko mkubwa kwenye maeneo ya masoko na maduka.  Huduma za usafirishaji nazo zitaendelea, wasafirishaji waendelee kuwaelimisha abiria, wale wakibaki kwenye viti magari yaende.”
 
Naye mgonjwa wa kwanza wa Corona Tanzania, Isabella Mwampamba akazungumza kwa njia ya simu na wana habari kutoka eneo alilotengewa kuhusu hali yake ya sasa.
 
(Sauti ya Isabella Mwampamba)

===================================================

2: Tukisalia nyumbani kujikinga na COVID-19, tusiwasahau wasio na makazi:UN

Wakati huu ambapo serikali zikitegemea watu kusalia nyumbani ili kusaidia kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya Corona, COVID-19 , ni lazima nchi zichukue hatua za kuzuia mtu yeyote kukosa makazi na kuhakikisha fursa ya mahali pa kukaa kwa wale wasio na makazi. Grace Kaneiya anafafanua zaidi

(TAARIFA YA GRACE KANEIYA)

Wito huo umetolewa leo na mtaalam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya makazi bora Leilani Farha ambaye ameongeza kuwa “Makazi yamekuwa ni silaha ya msitari wa mbele katika vita dhidi ya virusi vya Corona. Nyuma hivi sasa imekuwa ni muhimili baina ya hali ya maisha au kifo. “
Ameongeza kuwa kuna mambo yanayompa wasiwasi mkubwa “Nina hofu kubwa kuhusu makundi mawili ya watu, wale wanaoishi katika makazi ya dharura, wasio na makazi na makazi yasiyo rasmi, na pili wale ambao wanakabiliwa na kupoteza ajira na hali mbaya ya kiuchumi hali ambayo itasababisha changamoto ya kulipa mikopo ya nyumba, kodi ya pango na kukabiliwa na kufukuzwa katika makazi yao.”
Kwa mujibu wa mtaalam huyo takriban watu bilioni 1.8 duniani kote wanaishi bila makazi na kwenye makazi duni, na mara nyingi katika hali ya msongamano, wakikosa huduma za msingi kama maji na usafi na hivyo kuwafanya kuwa katika hatari ya kukabiliwa na virusi hivi vipya hasa kwa kuwa mara nyingi wanakabiliwa na changamoto nyingi za kiafya.
“Nitazitaka nchi kuchukua hatua zaidi kuhakikisha haki ya makazi kwa wote ili kuwalinda na zahma hii ya Corona.Kuna baadhi ya nchi wanachukua hatua nzuri ikiwemo kusitisha kuwafurusha watu wasiolipa kodi ya pango au kuchelewa kulipia mikopo ya nyumba hasa kule walikoathirika na virusi vya Corona, ambako majira ya baridi kali bado yanaendelea na kwa wale wanaoishi katika makazi yasiyo rasmi. Pia kuna wale wanaotoa huduma kama za maji safi na usafi kwa wasio na makazi tunaomba hili liendelee kwa wote.” Amesema mtaalam huyo.
Pia ameongeza kuwa wakati hatua muhimu zinahitajika kukabiliana na hatari ya makundi haya ya watu  na kushughulikia kiwango cha maambukizi mtaalam huyo maalum amesema ili kuhakikisha ulinzi kwa wasio na makazi au wanaoishi katika makazi duni “nchi lazima zisitshe kesi zote za kuwafurushwa makwao watu , ziwape makazi ya mud ana huduma za msingi wale waliathirika na virusi vya Corona na kuwatenga, kuhakikisha hatua za kudhibiti kama watu kutotembea hovyo hazisababishi adhabu kwa yeyote kutokana na hali ya makazi yake. Pia nchi zitoe fursa sawa ya upimaji na huduma za afya na pia kutoa nyumba kama inahitajika wakati wah aliya tahadhari na dharura ikiwemo kutumia nyumba zilizo wazi au kutelekezwa kwa ajili ya muda mfupi.”

 Kwa wanaokabiliwa na kukosa ajira

Na kwa wale wanaokabiliwa na kupoteza ajira na kukabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi kutokana na mlipuko huu wa Corona mtaalm huyo ana wito “ Nchi ni lazima zitoe msaada wa fedha kwa ajili ya kodi ya pangoo au kulipia mikopo ya nyumba, zisitishe hatua ya kuwafukuza watu kwa sababu ya malipo, zianzishe njia ya kupunguza kodi ya pango japo kwa wakati wa mlipuko na pia kusitisha kwa muda gharama za malipo ya matumizi mengine kama maji, umeme na gesi.

Amesema hadi sasa “Kuna hatua zimeshachukuliwa na fungu la fedha kutengwa ili kukabiliana na athari za kiuchumi zitakazosababishwa na Corona ikiwemo mdororo wa kiuchumi kama vile kupunguza kiwango cha riba. Hata hivyo amesema kuna hatari ya hatua hizo kutumika vibaya na kuitumia fursa za janga hili kutawala soko la nyumba bila kujali viwango vya haki za binadamu  kama ilivyofanyika wakati wa mdororo wa kiuchumi wa kimataifa mwaka 2008. Hivyo nchi lazima zizuie hulka hiyo ya taasisi na wawekezaji katika upande wa nyumba za makazi.
Amesisitiza kuwa “Kwa kuhakikisha fursa ya nyumba bora na usafi sio tun chi zitawalinda watu wake na kuokoa maisha ya wasio na makazi , bali pia zitasaidia kuilinda dunia dhidi ya COVID-19.


====================================================
STUDIO. MIDWAYSTING
====================================================
ASSUMPTA: Na punde ni makala ambapo leo tutakuwa nchini Kenya kuangazia hali ya kusambaa kwa virusi vya corona, hii leo nchi hiyo ikiwa imethibitisha kuwa na wagonjwa watatu wapya.
====================================================

3: Pamoja na COVID-19 mamilioni bado wahitaji misaada- OCHA
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya misaada ya dharura, OCHA imekumbusha kuwa mamilioni ya watu walio hatarini bado wanategemea misaada ya kuokoa maisha inayotolewa na Umoja wa Mataifa. John Kibego na taarifa kamili

(TAARIFA YA JOHN KIBEGO)

Naibu Msemaji wa OCHA Jens Laerke (TAMKA YENZ   LAKE)amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari mjini Grneva, Uswisi hii leo.

Bwana Laerke amesema kuwa baadhi ya nchi zilizokumbwa na virusi vya Corona au COVID-19 zilikuwa tayari kwenye janga la kibinadamu kutoka na vita, majanga ya asili na mabasiliko ya tabianchi.

Ameema ni muhimu dana kuendeleza kazi za kuokoa maisha katika hizo nchi na kwamba “tunaendeleza kazi za kibinadamu duniani kote.”

Kwa mujibu wa Bwana Laerke, “timu ya OCHA mjini Geneva zinasaidia uratibu, usambazaji wa taarifa na vifaa kwa ajili ya misaada ya kibinadamu na mashinani OCHA inasaidia nchi ambazo tayari zimekumbwa au zinaweza kukumbwa na COVID-19.”

Amesema ni muhimu sana kutomwacha yeyote nyuma katika janga la sasa na kwamba lazima kushirikiana kuishinda Corona.

Wakati huu ambapo bara la Ulaya ni kitovu cha COVID-19, “kila nchi bila kujali chochote lazima ichukue hatua za kijasiri kukomesha au kupungiza kasi ya maambukizi ya virusi vya Corona” amesema Hans Kluge, Mkuu wa WHO barani Ulaya.

 


===================================================
STUDIO: Play MUSIC 4 for 5 seconds and hold under
====================================================
ASSUMPTA:  Na sasa ni makala iliyoandaliwa na Jason Nyakundi nchini Kenya ambako sasa wagonjwa wa virusi vya corona wameongezeka na kufikia saba baada ya kuwepo kwa visa vipya vitatu. Visa ambavyo vimethibitishwa na waziri wa afya wa Kenya Mutahi Kagwe. Jason Nyakundi anasimulia zaidi.
=================================================
STUDIO: PLAY MAKALA
==================================================== 

ASSUMPTA: Play MUSIC 4 for 5 seconds and hold under
====================================================
ASSUMPTA:  

Shukrani Jason Nyakundi kwa makala hayo 
====================================================
Na sasa ni  mashinani tuungane na  Msemaji wa shirika la kuhudumia wakimbizi ulimwenguni, UNHCR, Cecile Pouilly akieleza jinsi shirika hilo  linasaidia wakimbizi  kujiepusha na virusi vya corona.
====================================================
Studio: Play Mashinani
====================================================
ASSUMPTA: 
Asante sana Cecile Poully kwa ujumbe huo.
==================================================
STUDIO: Play Bridge
ASSUMPTA: Na hadi hapo natamatisha jarida letu la leo. Hadi wakati mwingine kwa habari na makala kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa unaweza kupata matangazo na taarifa nyingine na kujifunza Kiswahili kwenye wavuti wetu news.un.org/sw. Msimamizi  wa matangazo ni FLORA NDUCHA na fundi mitambo ni……na mimi ASSUMPTA MASSOI, nasema kwaheri kutoka New York. 

==================================================
TAPE: CLOSING BAND

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
12'21"